Mabusha Kupeleka Watu Mahakamani

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza
limewahatarisha wananchi wa Tanzania kiujumla kuachana na vitendo vya
udhalilishaji kwa wanaume wenye mabusha kwa 'kuwajambisha' ama kuwapigia miruzi
kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi, Ahmed Msangi wakati akifanya
mahojiano na eatv.tv baada ya kushamiri kwa matukio mengi ya udhalilishaji na
unyanyasaji wa kijinsia licha baadhi ya watu kutofahamu kuwa wakifanya ni kosa
kwa mujibu wa sheria za nchi.
"Vipo
vifungu vya sheria vinavyoweza kumfikisha mtuhumiwa wa kitendo hicho Mahakamani
pamoja kutozwa faini kulingana na mfungua mashtaka atakavyokuwa anataka kulipwa
fidia kutokana na udhalilishaji aliyofanyiwa",amesema Kamanda
Msangi.



