Rais Magufuli: Baridi imeletwa na Mungu tuwajibike kujikinga na UKIMWI

Rais Magufuli Leo May 2, 2018
ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa hospital ya Kilolo ambapo amewataka
watu wa mikoa ya Njombe na Iringa kuchukua tahadhari juu ya gonjwa la UKIMWI
sababu mikoa hiyo ndio inayoongoza nchini.
“Mkoa wa Iringa na Njombe ina
maambukizi mengi ya UKIMWI, Iringa una 11.2% na Njombe ni 11.6%. Inawezekana
sababu ya msingi ni baridi lakini sina uhakika. Ni lazima tuwajibike katika
kujikinga na UKIMWI,” amesema Rais Magufuli.
“Kwahiyo Iringa ni ya pili Njombe ni
ya kwanza kwa maambukizi ya Ukimwi nilipofika hapa Kilolo inaonekana shida
kubwa hapa ni baridi na kwasababu inaletwa na Mwenyezi Mungu inabidi tujikinge
na kuchukua tahadhari zote kwa gonjwa hili.”Amesema Rais Magufuli.



