STARTIMES Kurusha Na Kutangaza Live Kombe La Dunia Urusi 2018 Kwa Kiswahili
Balozi
wa Startimes Tanzania kwenye msimu wa Kombe la Dunia na Msanii wa Bongo Movies,
Wema Sepetu akizungumzia namna walivyojipanga na wasanii wenzake wakati wa
kipindi chote cha Kombe la dunia wakishirikiana na Startimes Tanzania.
Meneja
masoko wa Kampuni ya Startimes, Bw. David Malisa akizungumza na waandishi wa habari
pamoja na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kurusha matangazo ya Kombe la
Dunia Urusi 2018 kwa kutumia lugha ya Kiswahili kwenye king’amuzi cha
Startimes.
Dar es salaam:
KAMPUNI
ya Star Media (T) Ltd yenye chapa ya StarTimes imetangaza rasmi kurusha
matangazo ya Kombe la Dunia Urusi mwaka 2018 Mubashara kupitia king’amuzi
chake. StarTimes imethibitisha kuonesha michuano hiyo leo katika hafla fupi
iliyofanyika Terrace, Slipway Masaki jijini Dar es Salaam na kushirikisha
waandishi wa Habari pamoja na wadau mbalimbali wa soka nchini.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Meneja Masoko wa Kampuni hiyo David Malisa amesema “Mwaka
huu katika Kombe la Dunia la 21, StarTimes ni mrushaji rasmi wa michuano hiyo
itakayoanza Juni 14 hadi Julai 15 nchini Urusi. Mechi zote 64 zitakazochezwa
Urusi katika Kombe la Dunia zitarushwa moja kwa moja.
”Amefafanua mbali na kurusha tu michuano hiyo maarufu zaidi Duniani, StarTimes
watarusha matangazo ya michezo yote katika lugha ya Kiswahili na hiyo ni katika
jitihada za kuienzi na kuikuza lugha ya Kiswahili lugha ambayo ni
maarufu zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
“StarTimes
tutarusha matangazo ya Kombe la Dunia, mechi zote 64 katika lugha ya Kiswahili
pamoja na uchambuzi utakaoambatana na mechi hizo, uchambuzi utakaofanywa na
wachambuzi mahiri na tuliowazoea hapa nchini”, alisema Bw. David.
Sambamba
na kuzindua Kombe la Dunia, StarTimes pia wametangaza ofa kwa wapenzi wa soka,
ambapo wateja watakaonunua king’amuzi au Luninga zao za kidigitali kati sasa na
Juni 30 watapatiwa kifurushi cha juu hadi Julai 31 mwaka huu bure.
Mkuu
wa Kitengo cha Maudhui ya Startimes, Zamarad Nzowa akizungumzia namna
walivyojipanga wakishirikiana na wasanii mbalimbali wa hapa nchini kwenye msimu
wa kombe la Dunia litakalochezwa nchini Urusi hasa kwenye vipindi
mbalimbali vitakavyokuwa vinarushwa kupitia kwenye king’amuzi cha
Startimes.
Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la utangazaji nchini Tanzania (TBC), Bi. Edna
Rajab akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni mbalimbali waliofika
katika uzinduzi wa kurusha matangazo ya Kombe la Dunia Urusi 2018 kwa kutumia
lugha ya Kiswahili kwenye king’amuzi cha Startimes.
Mchambuzi
wa Michezo, Jeff Leya akizungumzia fulsa aliyoipata mara baada kuingia mkataba
na Startimes kuchambua mpira kwenye kombe la dunia kupitia king’amuzi cha
Startimes.
Mkurugenziwa
Startimes Tanzania, Bw. Wang Xiaobo akipiga mpira golini kuashiria kufunguliwa
kwa uzinduzi wa kurusha matangazo ya Kombe la Dunia Urusi 2018 kwa kutumia
lugha ya Kiswahili kwenye king’amuzi cha Startimes.
Viongozi
wa Startimes wakiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii wakati wa wa uzinduzi wa
kurusha matangazo ya Kombe la Dunia Urusi 2018 kwa kutumia lugha ya Kiswahili
kwenye king’amuzi cha Startimes kwenye ukumbi wa Hotel ya Slip Way jijini Dar
es Salaam.




