Wema Sepetu Afunguka Kuhusu Kipindi Chake Wasafi Tv

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu
amefunguka na kuelezea mipango yake aliyonayo kuhusu kipindi
chake kinachotarajiwa kurushiana ndani ya Wasafi Tv.
Kama utakumbuka siku za nyuma kidogo Wema
aliweka wazi kuwa hana Mahusiano ya kimapenzi na Diamond bali atakuwa na
uhusiano wa kikazi naye kwani atakuwa bosi wake.
Wema alitangaza kuwa atakuwa na kipindi ndani
ya Wasafi Tv ambayo imeanza kurusha matangazo yake wiki chache zilizopita.
Wema amefunguka hayo kwenye press conference
aliyofanya kuweka wazi kitakuwa ni kipindi cha kawaida na sio reality show kama
ilivyokuwa mwanzoni kwenye EATV.
"Kitakuwa ni kipindi cha tofauti
tutakuwa wanadada watatu. Sitapenda kuweka wazi zaidi lakini haitakuwa reality
show, kama itakuwa ni reality show nitaweka kwenye App yangu.
"Bado hatujaanza ku-shoot kwa sababu
sasa hivi bado wanafanya majaribio, kwa hiyo ile process nzima ya vipindi bado
haijanza, so content zipo pale pale na tutaanza ku-shoot hivi karibuni”.



