Mhe Msigwa, DC Kasesela Warushiana Maneno 'Machafu' Mitandaoni Kisa Msiba Wa Mapacha

Siku moja baaada ya pacha
walioungana, Maria na Consolata kuzikwa, kumetokea mzozo baina ya Mbunge wa
Iringa Mjini, Peter Msigwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela katika
akaunti ya mtandao wa kijamii wa Twitter.
Mzozo ulianza jana Juni 6, 2018 baada ya Msigwa kuandika twiti
akisema: “DC Kasesela anafanya siasa kwenye msiba wa Maria na Consolata. Bila
aibu hajaacha kutaja jina langu akidhani kwa kufanya hivyo itamsaidia kisiasa.
Kasesela usitumie huo msiba kwa faida ya kisiasa. Shame on you! Umeshindwa hata
kumtambua Meya wa mji.”
Asubuhi ya leo Juni 7, 2018 Msigwa
ameandika tena twiti akisema: “DC Kasesela kila wakati is looking for
attention! niliwahi kusimuliwa watu wa aina hii! Kukiwa na harusi anatamani awe
bwana harusi! Kukiwa na ubatizo anatamani awe mbatizwaji! Kukiwa na msiba
anatamani awe jeneza. Boys are always looking for attention, men always have
attention.”
Akijibu hilo, Kasesela akaandika:
“Mheshimiwa Mbunge is this Real you?! Nimesema neno gani baya?”
Msigwa akaandika: “Umesema mbele ya
hadhara kuwa mimi sijatuma rambirambi ulijuaje? Kwani mimi nilipaswa kukupa
wewe ? Hao wabunge wa CCM hawajakuambia kama nilichangia! Kwani unadhani watu
wa Iringa hawamjui mbunge wao?”
Kasesela: “Omba re play you should
not stress yourself nimegundua hukunisikia umeambiwa.”
Msigwa: “Nimekusikia watu
walikushangaa sana unaposema eti Rita ni mbunge wa Iringa! Na walikupinga!
Umeshindwa kumheshimu Meya wa Mji! Hata wewe hustahili heshima.”
Kasesela: “Sasa Rita Kabati ni mbunge
wa wapi.”
Msigwa: “Acha ushamba”
Kasesela: “Mimi nimekubali ushamba
toka jana Kaka”
Msigwa; “Kwa Kweli washamba
wanaviherehere!”.








