TECNO POUVOIR 2 Uhakika Wa Chaji Ndani Ya Masaa 96.
Pamoja ya kuwa kampuni inayosifika katika
uzalishaji wa simu zinazotunza chaji, kampuni ya simu ya TECNO imeendelea
kudhihirisha ubora wake kwa mara nyengine tena kupitia TECNO pouvoir 2 (TECNO
LA7) ikiwa ni muendelezo wa ‘TECNO L series’ yenye betri 5000mAh na mtandao wa
4G.
pamoja ya kuwa na betri kubwa
aina ya Li-Polymer, 5V2A yenye kujaa chaji kwa haraka na kudumu nayo zaidi ya
siku tatu lakini bado kampuni ya simu ya TECNO hakusita kuhakikisha TECNO
pouvoir 2 inakuwa na muonekano mzuri kwa kupitia umbo lake jembamba la ‘metallic’
lenye kutawaliwa na wigo mpana wa kioo chenye uwiano wa 18:9.
TECNO pouvoir imebeba kamera
mbili nyuma ikiwa na megapixel 13 na flashi mbili za LED na mbele ikiwa na
megapixel 8 na LED flashi pamoja na mix flashi zenye kupiga picha nzuri na
zenye wang’avu kutokana na aina ya kioo cha TECNO pouvoir 2 kuwa na
upana wa nchi 6.0 HD+ (1440*720) 450nit IPS. Mix flashi inafanya kazi kama
ilivyo kwa flashi za kawaida isipokua yenyewe inapatikana ndani ya kioo cha
simu na inafanya kazi wakati wa kupiga ‘selfie’ tu.
Na ikiwa simu ya kwanza kwa
toleo la ‘TECNO L series’ kuwa na kasi ya mtandao wa 4G lakini pia TECNO
pouvoir 2 inaufanisi mzuri zaidi kutokana na processor ya MT6739WA 1.3 ghz
Quard-core pamoja na Android 8.1 Oreo na HiOS ya 3.3.
TECNO pouvoir 2 inatumia aina
tofauti tofauti za ‘security’ ikiwamo fingerprint inayopatikana nyuma ya simu
na face id yenye kunlock simu kupitia paji la uso na ndio simu ya kwanza ya
toleo la ‘TECNO L series’ kutumia face id.
Simu hii pia imekuja na memory
ya ndani ya GB 16 na GB 2 za ram vinavyoiwezesha simu kuhifadhi mafile mengi na
kufanya kazi zaidi ya moja kwa wakati mmoja pasipo kuathiri uwezo wa simu
lakini pia TECNO pouvoir inaweza kubeba hadi GB 64 memory ya ziada.
TECNO pouvoir 2 inapatikana
katika rangi tatu tofauti nyeusi, gold na city blue.
Kwa bahari zaidi tembelea
http://www.tecno-mobile.com/tz/index.php?id=740#/



