TIC Watanzania Jitokezeni Kuchangamkia Fursa Ujio Wawekezaji Nchini

Bw. Geoffrey Mwambe (wa pili kutoka kulia) akiinadi
Tanzania kwenye jopo la wataalamu wa uchumi walioongoza mjadala wa
upatikanaji wa mitaji, mazingira na fursa za uwekezaji ndani ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki wakati wa kongamano la Ujerumani na Afrika Masghariki, Berlin
Dar es salaam:
KITUO cha Uwekezaji nchini (TIC) kimewataka watanzania
kuchangamkia fursa ya ujio wa wawekezaji katika kujinufaisha kiuchumi na ukuaji
wa viwanda kwa kushirikiana nao kibiashara.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam Mkurugenzi
Mtendaji Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Geofrey
Mwambe wakati akitoa taarifa kuhusiana na ziara aliyofanya ya kikazi
nchini Ujerumani na Uholanzi kati ya tarehe 14 mpaka 17, Mei 2018 kutangaza
fursa za uwekezaji na kushawishi na kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza
nchini.
“Ni vyema wawekezaji wa hapa nchini wakajenga
uhusiano mzuri na wawekezaji kutoka nje ya nchi kwani ni jambo ambalo
litasaidia kuendelea kukuza maendeleo ya uchumi wa viwanda,” alisema Mwambe.
Alisema watanzania wanatakiwa kujitokeza kwa
wingi kujiunga na wawekezaji kutoka nje ili waweze kupata uelewa wa kutosha
katika ufanyaji wa biashara wa kimataifa lakini pia kufahamu mtu ambaye
wanataka kufanya naye biashara.
Bw. Mwambe aliongeza kuwa pamoja na kutokuwa
na mitaji ya kutosha, amewataka baadhi ya watanzania kuepukana na dhana ya kuwa
wawekezaji ni kutoka nje ya nchi pekee bali nao wanapaswa kuwekeza kwa kutumia
fursa zilizopo kwani mazingira ya uwekezaji ni mazuri.

Sehemu ya washiriki wa
kongamano la Biashara na Uwekezani kati ya Ujerumani na Nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki wakifuatilia mawasilisho ya mada ya juu ya hali ya uchumi kwa
nchi za Afrika Mashariki
taarifa kamili za Ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa
TIC Geofrey Mwambe katika nchi za Ujerumani na Uholanzi.
****
****
MKURUGENZI
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe amefanya
ziara ya kikazi nchini Ujerumani na Uholanzi kati ya tarehe 14 mpaka 17, Mei
2018 katika jitihada zake za kutangaza fursa za uwekezaji ili kushawishi
na kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini.
Akiwa
nchini Ujerumani Bw. Mwambe alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani
Mhe. Dkt. Possi Abdallah ambapo walifanya kikao cha kazi kabla ya kushiriki
kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Ujerumani na nchi za Afrika
Mashariki lililofanyika Mei 15, 2018 katika mji wa Berlin. Kongamano
liliandaliwa ili kutoa nafasi kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kunadi
fursa za uwekezaji kwa wafanyabiashara wa Ujerumani na dunia kwa ujumla

Mkurugenzi Mtendaji wa
Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Geoffrey Mwambe (kulia) alipomtembelea
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Dkt. Possi Abdallah ofisini
kwake Berlin, Ujeruman.
Vilevile
siku mbili baada ya kongamano, Kituo kilifanya ziara nchini Uholanzi ambapo
kilifanikiwa kusaini makubaliano ya mashirikiano (MOC) na Taasisi ya Biashara
za Kimataifa ya Uholanzi (DCIB) pamoja na kufanya mkutano na baadhi ya
wafanyabiashara wa Taifa hilo wenye nia ya kuja kuwekeza nchini. Sekta
zitakazohusika ni pamoja na mafuta, gesi, kilimo, afya, usafirishaji, viwanda,
fedha, mazingira, nishati na mawasiliano.

Pichani baada ya
kukamilisha zoezi la kusaini MOC . waliokaa kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TIC
Bw. Geoffrey Mwambe na kushoto ni Mwenyekiti wa DCIB Bw. Hans Biesheuvel.
Pamoja nao kulia ni Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji wa TIC Bw. John
Mnali,Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi Mhe. Irene Kasyanju,Mkurugenzi Mkuu wa
DCIB Dkt Dewanand Mahadew na Bi Zeinab Dauda Meneja wa DCIB Afrika Mashariki.
Makubaliano
yaliyomo kwenye MOC yatadumu kwa kipindi cha miaka mitano (5) na malengo yake
ni:
i. I/ kubadilishana taarifa
za fursa na mazingira ya uwekezaji
ii. kuratibu ujio wa wafanyabiashara wa
Uholanzi kuja Tanzania kuwekeza na kufanya biashara na Watanzania kwenda
Uholanzi
iii. II/ kujengea uwezo Kituo cha
Uwekezaji kufanya kazi zake za kutafiti, kuhamasisha na kufanikisha uwekezaji
iv. III/ kukuza sekta
binafasi ya Tanzania hususan wawekezaji wa ndani na wajasiriamali kupitia
mafunzo mbalimbali.
Kupitia
kongamano, Bw. Mwambe alielezea majukumu ya Kituo, msaada unaotolewa kwa
wawekezaji katika kuanzisha miradi, hali ya uchumi na mikakati mbalimbali
inavyotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi mahiri wa
Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa lengo la kuboresha mazingira
ya biashara na uwekezaji ili kuvutia uwekezaji wa mitaji ya kutoka nje (FDI).
Akiainisha
baadhi ya maeneo ambayo yanafanyiwa kazi na Serikali alisema ni pamoja na
kuweka mazingira wezeshi ya usajili wa biashara na leseni kwa wawekezaji wa
ndani na nje pamoja na kuondoa urasimu ndani ya mifumo ya Serikali kuanzia
ngazi ya Mtaa/Kijiji hadi Taifa ili kufanikisha utekelezaji wa miradi ya
uwekezaji kwa muda mfupi.
Bw.
Mwambe pia aliwahakikishia wawekezaji wa nchini Ujerumani na Dunia kwa ujumla
kuwa Tanzania ni nchi yenye fursa nyingi na mahali salama kwa uwekezaji ndani
ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika; hivyo wawekezaji wenye mitaji
na teknolojia wanakaribishwa kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ambazo
kwa sasa ni kipaumbele cha Taifa yaani viwanda, kilimo, madini, mifugo, uvuvi,
miundombinu, uzalishaji na usambazaji umeme na miundombinu kwa ujumla.
Nae
mwakilishi wa Benki ya Stanbic kwa Kanda ya Afrika Mashariki Bw. Jibran
Qureishi alieleza kuwa kwa sasa Tanzania inafanya vizuri katika masuala ya
Kiuchumi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Matokeo
hayo chanya ni kutokana na uongozi mahiri wa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe
Magufuli aliyeanzisha vita ya kupambana na rushwa; na kupunguza urasimu kwa
lengo la kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa
TIC Bw. Geoffrey Mwambe alipomtembelea Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe.
Irene Kasyanju ofisini ,The Hague, Uholanzi.
Bw.
Qureishi ambaye ni mchumi mbobezi aliweka bayana kwamba Tanzania ina nafasi
kubwa ya kuendelea kufanya vizuri zaidi katika nyanja ya uchumi kwa miaka ya
hivi karibuni baada ya kukamilika kwa miradi mikubwa ya maendeleo
inayotekelezwa na Serikali kwa kutumia rasilimali za ndani na sio mikopo
kama ilivyokuwa imezoeleka.
Moja, kwa upande wa Ujerumani
tumekutana na makampuni ambayo yameonesha nia ya kuwekeza kwenye sekta za
viwanda, afya, ujenzi, miundombinu, mawasiliano, usafirishaji na nishati.
Pili, kuanza kwa utekelezaji wa makubaliano ya
ushirikiano kati ya Kituo na Taasisi ya Biashara za Kimataifa ya Uholanzi
kunatoa fursa ya kutekelezwa masuala mbalimbali kwenye miradi ya ubia,
upatikanaji wa fedha za miradi, uhamishaji wa teknolojia na ujuzi, kuandaa
semina /warsha na misafara ya wawekezaji. Kituo kinatarajia kupokea kundi la kwanza
la wafanyabiashara kutoka Uholanzi mapema mwaka 2018/2019.
Tatu, kwa upande wa Uholanzi
tumekutana na makampuni yaliyoonesha nia ya kuwekeza kwenye sekta za utalii,
ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza spea za magari, uanzishaji wa chuo cha
mafunzo ya ufundi (Vocational Training), uanzishaji wa mradi wa usimamizi wa
usalama wa mizigo kuanzia bandarini mpaka eneo husika na usimikaji wa mitambo
ya kutengeneza bidhaa mbalimbali za ngano.
Kwa
upande wake Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju amesema
kusainiwa kwa makubaliano kati ya TIC na DCIB ni hatua kubwa ambayo
itarahisisha utekelezaji wa sera, diplomasia ya uchumi. Mhe. Balozi
amehitimisha kwa kuhimiza wadau wa sekta binafsi ya Tanzania kutumia vema
makubaliano hayo kama fursa ya kuongeza biashara na uwekezaji kwa kushirikiana
na wadau kutoka Uholanzi.



