Breaking News

Mhungaji MASHIMO Ashtukia Rafu Aomba kumwona Jaji Mkuu Kiongozi.

MCHUNGAJI wa Mitume na Manabii na Maaskofu Tanzania wa kanisa la Emmaus Bible Church Pentecostal Komando Mashimo ameomba kumuona Jaji Mkuu Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Ombi hilo amelitoa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam akilalamikia mmoja wa Maajaji wa Mahakama hiyo kwa kudai kuwa hakumtendea haki katika shauli lake la madai ambalo kampuni yake iliifungulia kampuni ya Msanii Maarufu wa Filamu nchini Richi Mtambalike.

“Nilimshitaki katika mahakama ya Kinondoni, kwani aliingia na mimi mkataba kwa ajili ya kazi yangu lakini baadae akanitapeli ndipo nikafungua shauli, kesi ikawa inasikilizwa lakini nilishangaa kesi yangu kutupiliwa mbali pasipo sababu ya msingi,” alisema Mashimo.

Alidai baada ya kesi hiyo kutupiliwa mbali aliamua kukataa rufaa mahakama kuu nakesi ikaendelea kusikilizwa lakini alikuja kusikia hukumu ya kesi hiyo mtaani ikielezwa kuwa mdaiwa ameshinda.

Aidha alisema kuwa ameamua kuomba kuonana na Jiji huyo kupitia vyombo vya habari baada ya juhudi zake kugonga mwamba kwani aliomba viongozi wa mahakama ruhusa ya kuonana naye lakini alinyimwa nafasi hiyo.

Katika madai hayo Mashimo anadai kuwa ametapeliwa sh.milioni 80