Breaking News

Mahakama Kuu Kesho Kuamua Juu Ya Uhalali WA Lipumba Ndani Ya CUF Shauri Namba 23/2016.

KESHO TAREHE 30/11/2018 MAHAKAMA KUU KANDA YA DARE ES SALAAM MBELE YA MHESHIMIWA JAJI DKT. MASOUD MUSSA BENHAJJ, Inatarajia kutoa Uamuzi juu ya uhalali wa Msajiri wa Vyama vya siasa nchini Jaji Franscis Mutungi kumuandikia barua ya kumtambua LIPUMBA kama Mwenyekiti Halali wa CUF na hivyo kumpa Kibali cha kurejea Ofisini kuendelea na majukumu yake ambapo aliutekeleza uamuzi Tarehe 24/9/2016 kwa kufanya uvamizi wa Ofisini Kuu buguruni akiambatana na kundi la vijana wahuni huku akipata (full support) msaada toka kwa Jeshi la Polisi, baada ya muda wa Mwaka mmoja (Takriban miezi 14) kuwa nje ya Ofisi na utendaji wa shughuli za Chama.

Itakumbukwa kuwa Tarehe August 6, 2015 Peacock Hotel-Dar es Salaam, Lipumba alizungumza na Waaandishi wa Habari na kupitia kwao kuzungumza na Watanzania na Dunia kwa ujumla kuwa AMETANGAZA RASMI KUNG’ATUKA/KUJIUZULU nafasi ya Uenyekiti wa Chama Cha CUF Taifa. 
Lipumba alieleza kuwa “LEO HII NIMEIKABIDHI OFISI YA KATIBU MKUU, BARUA YANGU YA KUNG’ATUKA NAFASI YA MWENYEKITI WA TAIFA, LAKINI NAENDELEA KUWA MWANACHAMA WA CUF NA KADI YANGU IMELIPIWA MPAKA MWAKA 2020.  Katika kipindi cha kabla ua Uchaguzi Mkuu nitajishughulisha na kuandaa ushauri wa mambo yanayopaswa kufanywa na serikali ijayo ikiwa ni pamoja na; (rejea Taarifa yake hapo chini) …Baada ya Uchaguzi nitajikita katika kufanya utafiti na kutoa ushauri kuhusu maendeleo ya uchumi shirikishi wa Taifa letu”

“Nawashukuru wanachama wa CUF na wananchi kwa ujumla kwa kuniunga mkono WAKATI NIKIWA KIONGOZI WA CHAMA HIKI. NAWAOMBA RADHI SANA WANACHAMA NA WANANCHI WALIOAMINI NA KUONESHA MAPENZI MAKUBWA KWANGU NA KATIKA UONGOZI WANGU. KATIKA HALI HALISI ILIYOPO NDANI YA UONGOZI WA CHAMA CHETU MIMI NAONEKANA NI KIKWAZO NA KWA HIYO SIWEZI KUWA NA MCHANGO WA MAANA KAMA MWENYEKITI KATIKA MAPAMBANO YA KUDAI HAKI SAWA KWA WOTE KATIKA KIPINDI HIKI.” 

Ilisema sehemu ya mwisho ya taarifa yake kwa Vyombo vya Habari na Umma kwa ujumla.

Mwaka mmoja Baadae June 13, 2016 akiwa Ofisi ya CUF Buguruni alipoomba na kukaribishwa kufanya Mkutano na Waandishi wa Habari aliodai kuzungumzia UCHAMBUZI WA BAJETI KUU YA SERIKALI 2016/2017 pamoja na mambo mengine akatangaza Kurejea tena kwenye nafasi hiyo, ENDAPO CHAMA HICHO KITAKUBALIANA NA OMBI LAKE. Alisema kuwa, anarejea kwenye nafasi hiyo baada ya muda wa kutosha aliyotumia kutafakari siasa za nchi na namna demokrasia inavyokanyagwa na watawala. Alisema amemuandikia barua Katibu Mkuu wa CUF, akimjuilisha kwamba AMETENGUA UAMUZI WAKE WA KUJIUZULU UENYEKITI WA CHAMA. 

“Nimemwandikia Katibu Mkuu (Maalim Seif Sharif Hamad) kutengua barua yangu niliyoandika tarehe 5 Agosti mwaka jana,” “Sasa nasubiri majibu kutoka kwa Katibu Mkuu baada ya barua yangu kujadiliwa na ngazi husika za chama.” Katiba ya mwaka 1992 Toleo 2013 Ibara ya 117(2) inaeleza kwamba, barua ya kujiuzulu inapaswa kujadiliwa na Mkutano Mkuu wa Chama, jambo ambalo mpaka sasa halijafanyika. alisema Lipumba. 
Lipumba alisema dhuluma iliyofanyika Zanzibar ya kuporwa kwa haki ya wananchi, imemsukuma kurejea kwenye mapambano ya haki nchini. 
“Rais Magufuli asipozingatia misngi ya kidemokrasia nchi haitakuwa na uwajibikaji.” 
Bado demokrasia Tanzania ina matatizo akitoa mfano wa bunge kuendeshwa kwa itikadi ya chama. Alisema kwamba UONGOZI WA RAIS MAGUFULI UNAONEKANA KUWA WA KASI INAYOPINGANA NA DEMOKRASIA. 

Kuhusu Zanzibar, alisema CUF na Watanzania wapenda haki hawautambui utawala wa Zanzibar wa Dk Ali Mohamed Shein kwa kuwa hakupatikana kwa njia halali.

Haya ndiyo baadhi ya kauli/maelezo ya Lipumba aliyoyatoa wakati wa kujiuzulu na wakati anataka kurejea katika nafasi aliyoiacha kwa kujiuzulu.

Fuatilia kuona kauli hizo alizozitoa kama alizisimamia na kama kuna ukweli ndani yake anaouishi juu yake. Leo anakunywa Chai Ikulu na Dkt Shein. Na kuunga mkono juhudi za kuuwawa kwa misingi ya Haki, usawa na Demokrasia ndani ya JMT. 

Hata hivyo;
• Mkutano Mkuu Maalumu wa CUF uliofanyika Blue Pearl Hotel Tarehe 21/8/2016 ulikubali KUJIUZULU KWAKE KWA KURA ZA WAJUMBE 476 NA WAJUMBE 14 KUKATAA NA WAJUMBE 128 HAWAKUPIGA KURA YA KUKUBALI AU KUKATAA.

• Baada ya Uvamizi wa Ofisi Kuu alioufanya Lipumba, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF liliazimia kutumia njia za kisheria kudai haki iliyoporwa na Lipumba akisaidiwa na washirika wake. Na kukubaliana kutotumia njia za Vurugu na uvunjifu wa Amani.

• Matukio mengi yaliendelea kujitokeza baadae ikiwa ni pamoja na Kuchota fedha za Ruzuku ya CUF kinyume na Sheria, kufukuza Viongozi, Madiwani na Wabunge wa CUF, kuunda Vyombo FEKI vya Maamuzi ikiwemo Bodi ya Wadhamini, kuwafarakanisha wanaCUF miongoni mwao na kuchochea mpasuko, Lugha zisizo na staha kutumika, wanachama kushambuliwa Mahakamani, majaribio ya kuteka Viongozi  na kujaribu kupandikiza chuki kati ya walichokiita ‘Utanganyika’ na ‘Uzanzibari’, kuitisha Uchaguzi FEKI wa ndani ya Chama, Nakadhalika.

KESHO panapo majaaliwa na kama hakutakuwa na dharura yeyote ile,  MAHAKAMA KUU inakwenda kuamua juu ya suala hili kama ni Halali kutengua kujiuzulu au la. Kama ni Halali Msajili kumrejesha Lipumba au la, hayo na mengine mengi TUTAYAJUA. Awali shauri hili lilikuwa litolewe uamuzi Tarehe 12/10/2018.

HAKI SAWA KWA WOTE

MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI HABARI,
maharagande@gmail.com 
+255 715 062 577
+255 767 062 577