NEC Yaongeza Muda wa Siku Tatu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoa wa Dar

Tume ya taifa ya uchaguzi NEC imeongeza muda wa siku tatu zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza mapema leo 20 February jijini Dar es salaam, mkurugezi wa uchaguzi NEC, Dkt. Wilson Charles alisema zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura litaendelea mpaka tarehe 23 February 2020.
"Kwa mujibu wa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 15(1) cha sheria ya Taifa ua uchaguzi, sura namba 343 na kifungu cha 21(1) cha sheria za serikali za mitaa sura namba 292 tume ya taifa imeamua kuongeza siku tatu hivyo zoezi la hilo litakamilika terehe 23 February 2020" Alisema Dkt. Charles.
Alisema katika muda huu wa nyongeza zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura litaendelea na vituo vyote vitaendelea kuandikisha kama awali kwa kufunguliwa sa 2 asubuhi na kugungwa sa 12 jioni.
Aidha Dkt. Charles ametoa wito kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam kuutumia vizuri muda huu wa nyongeza kwa kujitokeza kwa wingi hili taatifa zao ziweze kuingizwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kwani hakutakuwa na mda mwingine wa nyongeza katika awamu hii ya kwanza.