Breaking News

Prof. Lipumba Atolea Ufafanuzi Ripoti ya CAG.

Chama cha wananchi CUF kimetoa ufafanuzi juu ya ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) ya mwaka 2018/19 iliyowasilisha kwa rais Mhe John Magufuli kuhusu matumizi ya fedha za rizuku za chama hicho zaidi ua milion 369.

Akizumza makao makuu ya chama hicho buguruni jijini Dar es salaam Mwenyekiti CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba alisema kauli hiyo ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali imesababisha kuwepo na sintofahamu kubwa kuhusu usimamizi wa fedha za chama.

"Napenda kutoa ufafanuzi juu ya tuhuma zilizotolewa na CAG Charles Kichele kwa kuanza kuweka rekodi sawa juu ya tuhuuma alizozitoa za kupokea rudhuku milioni 369.38 kutoka serikali na kuamishwa kwa kiasi cha shilingi milioni 300 kwemda katika akaunti binafsi"

Alisema wakati tikio hili likitokea mwaka 2017 chama kilikuwa katika mgogoro mkubwa wa uongozi jambo lilopelekea akaunti za chama katika benki ya NMB kuwekewa tishio la kuzuwiwa.

Kufatia kuwepo kwa tishio hilo na ikumbukwe pia tayali tume ya taifa ya uchaguzi NEC tayali ilikiwa imeshatangaza uchaguzi mdogo wa marudio katika kata 20 tanzania bara pamoja na ule wa jimbo la dimani Zanzibar.

Kufatia tangazo la NEC chama kilimwandikia barua msajili wa vyama nchini Dec 28, 2016 kumwomba aidhinishe ruzuku yankila mwezi ya chama kutoka serikalini hili kiweze kujiandaa kushiriki uchaguzi huo pamoja na mipangoa ya ujenzi wa chama ambapo msajili aliridhia ombi hilo.

"Kufatia msajili wa vyama kuridhia barua yetu ya kuomba sehemu ya ruzuku ya chama na kipindi hicho chama kilikuwa katika mgogoro na aliyekuwa katibu mkuu wake hivyo kuzuia akaunti zote kamati ya utendaji iliamua shilingi milioni 300 zilizoombwa kugharamia uchaguzi ziamishwe kwenda katika akaunti ya mwanachama muaminifu ili zisije kukwama" Alisema Prof Lipumba.

Katika hatua nyingine Profesa lipuma ametoa ushauri kwa CAG kuimalisha udhibiti wa fehda za ndani ya chama iimarishwe kwa kufata sheria na katiba za chama husika hili kusaidia kuzuia ubadhilifu wa fedha hizo.