Rc Makonda Awataka Wananchi kuacha Mamlaka ya kutangaza Mgonjwa wa Corona

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda amesema Mwananchi wa kawaida hana ruhusa ya kutangaza kuwa mtu ana Coronavirus kisa umemuona Hospitali kwani Mamlaka hayo anayo Waziri wa Afya, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais
Akizungumza katika ziara ya kutembelea kujionea namna viwanda vilivyojiandaa kuzalisha bidhaa za kukabilia na ugonjwa huo jijini dar es salaam alisema kumezuka tabia baadhi ya kujitangaza katika mitandao ya kijamii jambo ambalo linaweza kuongeza hofu kwa wananchi.
"Mkoa wangu ndio unaongoza kwa wajuaji, sasa niwaombe msilete ujuaji, kwenye hili janga la COVID19, tujifanye wajinga kidogo ili tupone. Hata kama una mpenzi wako hamjakutana mwezi mzima vumilia.”Alisema Mhe. makonda.
Alisema katika kukakikisha ugonjwa huo unapatiwa ufumbuzi tayali ameshafanya mazungumzo na serikali ya watu wa Uchina kuwaomba msaada wa vifaa vya kupimia na wamekubali kutusaidia.
"Tayali nimefanya mazungumzo na balozi wa china nchini kuweza kusaiidiwa vifaa hili kuweza kupima na CORONA balozi wamekubali kutusaidi tayali vifaa ivyo vipo njian kuja Jijini Dar muda si mrefu kwani amewasiliana na Watu wa China kupitia kwa Balozi na wamekubali kuleta vifaa hivyo
Katika hatua nyingene Rc Makonda amemuomba Wazira wa Fedha, Philip Mpango kuangalia uwezekano wa kupunguza au kuondoa kodi kwa malighafi kutoka nje zinazotumika kutengeneza Sanitizer ili kuhakikisha viwanda vyetu vinaendelea kutengeneza na zikauzwa kwa bei nafuu
"Nimwombe waziri wa fedha kupunguza kodi au kufuta kabisa kwa malighafi ambazo zinatoka nje ya nchi kutengenezea Sanitizer hili kuwezesha bidhaa hiyo muhimu katika kipindi hiki kuweza kupatijana kwa bei nafuu ambayo itamwezesha mwananchi wa kawaida kuweza kuhimudu" Alisema.



