Tamasha la MAZAUG Lunch Party kufanyika Sept 6 Jijini Dar

Jumuuiya ya Kiislamu ya MAZAUG Tanzania imeandaa tamasha la MAZAUG LUNCH PARTY ambalo litafanyika tarehe 6 Septemba katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.
Akizungumza jijini Dar es salaam mratibu wa tamasha hilo bw. Fadhili Fakhair Massanza alisema leo la tamasha la Mazaug lunch party ni kutoa burudani na ujumbe kwa jamii kupitia mziki wa qaswida.
"Lengo kubwa la kuandaa tamasha hili ni kutoa ujumbe kwa jamii kupitia mziki wa qaswida pamoja kutoa elimu za kujitambua, mahusiano na uchumi kwa washiriki"
Alisema tamasha hilo pamoja na kutoa burudani pia limekuwa mstari kufanya shughuli mbalimbali nchini zilinazolenga kuijenga jamii ya kitanzania.
Aidha bw. Massanza aliongeza mgeni rasmi anatarajiwa kuwa shekh mkuu wa mkoa wa dar es salaam Alhad Mussa Salum pamoja na sheikh Hilal kipozeo ambao watatoa miadhara na mafunzo mbalimbali.
"Napenda kutoa wito kwa eaislam na wananchi wa mkoa wa dar es salaam kujitokeza kwa wingi siku hiyo wao na hata na familia zao kwani ni sehem sahihi ambayo inafaa kuja na familia na kuweza kujifunza wote kwa pamoja.



