Wanafunzi Kutoka Vyuo Vikuu 15 Wachangia Damu.. pamoja na Kutoa Msaada Kwa Watoto Hospirali ya Muhimbili
Mmoja wa wanafunzi akifanyiwa vipimo tayali kwa kuanza zoezi la kutoa damu katika hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Afisa kutoka kitengo cha Damu Salama hospitali ya taifa Muhimbili bw. John Bigamalaye akitoa elimu juu ya umuhimu wa kutoa damu katika hafla hiyo ya uchangiaji damu iliyoandaliwa na wanafunzi wa vyuo vikuu 15 nchini katika hospital ya taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Watoa huduma kutoka kitengo cha damu salama hospitali ya taifa muhimbili akiendelea na zoezi la kuchukua vipimo tayali kwa kuanza zoezi la uchangiwaji wa damu katika hafla iliyofanyika katika hospitali ya taifa muhimbili.
Balozi chuo kikuu cha Ardhi Prince Gasper Ivo akizungumza mara baada ya kuchangia damu katika hafla ya kuchangia damu iliyoandaliwa na wanafunzi wa vyuo vikuu 15 na kufanyija katika hospitali ya taifa Muhimbili 8 Agust 2020.








