KCB Benki Kuendelea Kutoa Huduma Bora Kwa Kila Mtanzania.

Banki ya KCB imezindua wiki ya huduma kwa wateja kwa kuwezesha wateja kupata huduma na ushauri juu ya huduma mbalimbali ambazo zinatolewa na benki hiyo nchini.
Akizungumza katika ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja mkurugenzi wa benki hiyo bwana Cosmas Kimario alisema katika kipindi chote cha wiki ya huduma kwa wateja watapata ushauri juu ya huduma zinazotolewa na benki hiyo.
"katika wiki hii ya huduma kwa wateja wateja benki yetu watapata wasaa wa kuuliza na kupatiwa ufafanuzi juu ya huduma zote zinazotolewa na benki kwa lengo la kuahakikisha tunawapatia wasaa wateja wetu wa kutambua huduma zetu"
Alisema katika wiki hii ya huduma kwa wateja benki ya KCB inaendelea kuakikisha kusogeza huduma zake karibu zaidi kwa wateja sambamba na kuendelea kutoa huduma zenye viwango vya hali ya juu ambazo zinakidhi hali ya kila mtanzania.

Kwa upande wake Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na mahusiano Bi.Chiristina Manyanya alisema katika wiki ya huduma kwa wateja benki hiyo itajikita pia katika kufanya matukio ya kijamii kwa kutoa misaada kwa vituo vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na kuandaa mechi ya kirafiki.
"Katika wiki hii ya huduma kwa wateja benki ya KCB itatoa misaada kwa vituo vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na kuandaa mechi ya kirafiki"

kwa upande wake mteja wa benki hiyo Bi Diana Metta ametoa pongezi kwa uongozi wa benki hiyo kwa kuendelea kuwaa wabunifu na kutoa huduma zilizo bora na zenye viwango ambazo zinaweza kutumiwa na kila mtanzania.



