Breaking News

Mgombea Urais ADC QUEEN SENDIGA Aahidi Kurudisha Kiwanda Cha Kuzalisha GESI

Mgombea Urais kupitia chama cha ADC Bi. QUEEN SENDIGA amesema kama atapatiwa ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Rais wa jahuri ya Muungano wa Tanzania atarejesha kiwanda chaa kuzalisha Gesi mkoani mtwara

"Nikipata ridhaa na kura zenu za kutosha tarehe 28  nawaahidi kurudisha kiwanda cha kuzalisha gas hapa hapa Mtwara ili Watoto wetu, vijana wetu nao wanufaike na rasimali hii Mungu aliyetuzawadia " 
Ameyasema hayo Akiwa kusini Mwa Tanzania katika kijiji cha Nanyagaa wilaya Tandahimba katika muendelezo wa kampeni zake za kata kwa kata. kijiji kwa kijiji. Mgombea huyo wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  amehitimisha kampeni zake katika wilaya Tandahimba
Leo ataendelea na kampeni zake Wilaya ya Rufiji, Kibiti na Mkuranga