Breaking News

KABENDERA Ataja Viapumbele Vyake Kama Atachaguliwa Kuwa Mbunge Jimbo la Ubungo

Mgombea ubunge wa jimbo Ubungo kupitia Chama cha Ukombozi CHAUMA Bw. kabendera Eugene amesema ikiwa atapatiwa ridhaa ya kuwa mbunge wananchi wa ubungo katika kipindi cha siku 100 baada ya kuapishwa ataakikisha wanafunzi wanapata Chakula shuleni pamoja na kuboresha huduma ya chakula katika Hospital za Umma.

Akizungumza jijini Dar es salaam juu ya vipaumbele vyake ikiwa atapatiwa ridhaa na kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo katika kipindi cha miaka 5 ya uongozi wake.

Alisema swala la kutoa chakula kwa wanafunzi ni jbo la msingi sana kwa ukuaji wa mtoto kiakili na kimwili ivyo atakapo chaguliwa na wana ubungo atahakikisha analifanyia kazi kwani uwezo wa serikali kufanya hivyo inao.

"Ikiwa nitapatiwa ridhaa yaa kuchaguliwa ntahakikisha wanafunzi wanapata huduma ya chakula awapo shuleni na wagonjwa hosptalini kwa kuhakikisha wanapagiwa huduma ya chakula"

Aidha bw kabendera amevitaja vipaumbele vingine kuwa ni pamoja na kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana kwa kuakikisha anafufua viwanda akitolea mfano kiwanda cha urafiki ambacho kikifufuliwa kitatoa ajira nyingi na za uhakika.

Ametaja kipaumbele kingine kuwa ni kupeleka hoja binafsi hili mikopo ya halmashauri iweze kuwezesha vijana wengi zaidi tofauti na ilivyo sasa kufatia vijana wengi kushindwa kuchangamkia mikopo hiyo kutokana na kuwepo vikwazo vingi husasani riba.

Pia bw. Kabendera ametaja kipaumbele ambacho atahakikisha akipatiwa ridhaa ni kutatua changamoto ya hostel kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vinavyopatikana  jimboni humo kwa kuhakikisha anatengeneza mazingira bora kwa wanafunzi hao kupata sehemu nzuri za hostel na kwa gharama nafuu.