Breaking News

SHOMARI KIMBAU:Maandalizi Ya Pambano La kimataifa Kati ya Twaha Vs Lamthuan Yamekamilika

Maandalizi ya pambano la Ngumi la kimataifa la uzito wa Silver Super Middleweight kati ya Twaha Ruaha wa Tanzania na Sirimongkhon Lamthuan kutoka nchini Thailand yamekalika na pambalo hilo litafanyika 30 Octoba katika ukumbi wa PTA sabasaba.
Akizungumza na waandishi wa habari mratibu na muandaaji wa pambano hilo Shomari Kimbau alisema maandalizi yote ya pambano hilo la kimataifa la  yamekamilika.

"Napenda kuwafahisha wakkazi wa jijini la Dar es salaam na mikoa ya jirani ule mpambano wa kimataifa ambao walikuwa wanaungoja kwa hamu kubwa maandalizi yote yamekamilika na hivyo wajitokeza kwa wingi siku 30 octoba kushuhudia pambano hilo kubwa"

Alisema pambano hilo kali na la aina yake tayali limeshadhibitishwa pia na WBC Asian Boxing Council kuwepo wa pambano hilo.

Aidha bw. Kimbau aliongeza kuwa siku hiyo pia kutakuwepo na mapambano ya utangulizi ambayo yatawakutanisha mabondia wakali zaidi ya watano.
"Siku ya tarehe 30 Octoba kutakuwepo na mapambo ya utangulizi kwa kuwakutanisha mambondia wakali kabla ya kuanza kwa pambano hili la kimataifa"

Amewataja mabondia hao kuwa ni Alphonce Tumbo ambae atazichapa na Jongo Jongo,  Maono Ally ambae atazichapa na Joseph Sinkala pamoja na Said Juma dhidi ya Ibrahim Tamba.

Amewataja wengine ni Saidi Wingo ambaye ataIchapa na Francis Miyeyusho,  Hamza Iddy na Jamal Kunoga pia wadada Ruth Chisale atazichapa na Sijali Saidi.