MUSIBA: Atoa Taadhali Kwa Mhe LISSU Kuacha Kukashifu Rais MAGUFULI

Mwanaharakati Cyiprian Musiba amemuonya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu kuacha tabia ya kumkashifu na kumtoa maneno ya kejeli kwa Rais Dkt John Magufuli.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam juu ya mwenendo wa kampeni zinazoendelea za kunadi sera za wagombea kiwa zimebaki siku chache wananchi kupiga kura ya kuchagua viongozi wa kuwaongoza kwa miaka tano Oktoba 28, 2020.
Aliema kumekuwepo na matukio ambayo yamekua yakiendelea ambayo yanatakiwa kukemewa na kila anayependa amani na mshikamano tulionao kufatia kauli ambazo amekuwa akizitoa mhe. Tundu Lissu kila anaposimama kwenye jukwaa kazi yake ni kumtukana Rais Dkt John Magufuli badala ya kutangaza sera za Chama chake na jinsi atakavyo waongoza watanzania.
“Asione kama Rais Dkt John Magufuli hana watu wanaomsapoti, tupo tena wengi na matusi yake hayavumiliki akiendelea nitamshughulia namuomba Mwenyekiti wake wa Chama Freeman Mboe amzuie “Alisema Musiba.
Alisema tatizo la ajira lipo duniani kote sio Tanzania tu hivyo aache tabia ya kuwadanganya watu kua yeye anakuja kutatua changamoto ya ajira.
Aidha Bw. Musiba amewataka watanaznia kuwapuuza wanaobeza kazi kubwa iliyofanywa na Rais Dkt John Magufuli kwani anapaswa kupongezwa na sio kukashifiwa wala kudharauliwa.



