Breaking News

BREAKING NEWS: SERIKALI YAYAFUNGULIA MAGAZETI YA MWANAHALISI, MAWIO, MSETO NA TANZANIA DAIMA

Serikali imeyafungulia rasmi magazeti ya Mwanahalisi, Mawio, Mseto na Tanzania Daima yaliyokuwa yamefungiwa kwa muda mrefu.

Uamuzi huo umetangazwa leo Alhamisi Februari 10, 2022 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye wakati akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na kutoa leseni ya magazeti hayo.

"Agizo la Rais ni Sheria,  Leo hii natoa Leseni kwa Magazeti manne ambayo ni Mwanahalisi, Mawio, Mseto na Tanzania Daima. Mama kasema Kazi Iendelee tuanze ukurasa mpya" , Alisema mhe. Nnauye.

Akizungumza mara baada ya kupokea leseni mmiliki wa magazeti ya Mwanahalisi na Mseto, Said Kubenea amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu kwa kufungua ukurasa mpya na vyombo  vya habari huku akisisitiza kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali.