GSM YAJTOA KUWA MDHAMINI MWENZA NBC PREMIER LEAGUE
Kampuni ya GSM imetangaza kujitoa rasmi katika nafasi ya kuwa mdhamini mweza wa ligi kuu ya NBC Premier league kuanzia leo February 7 kufatia kutokutekelezwa kwa baadhi ya vipengere vya kimkataba.
Akitangaza uamuzi huo Afisa Biashara Mkuu wa kampuni hiyo Bw. Allan Chonjo alisema sababu kubwa kutishwa kwa mkataba huo ni kufatia shirikisho la mpira nchini pamoja na bodi ya ligi kushindwa kushindwa kutekeleza vipengere vya mkataba kama pande mbili zilivyokubaliana.
"GSM ilishawishika sana kuwa mdamini mwenza wa ligi kuu ili kukuza sekta ya mpira wa miguu pamoja na michezo kwa ujumla nchini lakini hili halikwenda kama lilivyokusudiwa" Alisema bw Chonjo.
Alisema maamuzi haya si maamuzi rahisi kwani GSM inatambua kuwa vipo baadhi ya vilabu vya mpira vitakavyoumizwa pamoja na wadau ila aikuwa dhamira ya kampuni kufikia uamuizi huu.
Bw Njojo aliongeza kuwa GSM inapenda kushukuru TFF, Bodi ya ligi, vilabu pamoja na wadau wote kwa ushirikiano na kuwezesha kuwa sehemu ya kuendeleza sekta ya ya michezo nchini.
Aidha aliongeza kuwa kwa niaba ya Ghalib Said Mohammed, ambaye ni mwenyekiti na mjumbe wa kamati ya ushindi wa timu ya Taifa (Taifa Star) amefanya maamuzi magumu ya kujiuzulu nafasi ya mwenyekiti pamoja nafasi ya mjumbe wa kamati hiyo kuanzia leo.



