JATU PLC YAMTANGZA MSANII MRISHO MBOTO KUWA BALOZI WAKE.
Kampuni ya JATU PLC imemtangaza Msanii Mrisho Mpoto kuwa Balozi wa Kampuni hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu pamoja na kuandaa kipindi maalumu kitakachoitwa" (Kaa Hapa Awamu ya Pili) kitakachokuwa kikitangaza na kuelezea miradi mbalimbali ya iliyofanywa na serikali ya awamu ya sita katika sekta zay Kilimo, Ufugaji, Maji, Ujenzi na Utalii.
Akizungumza katika hafla ya kutiliana saini jijini Dar es salaam, Meneja Mkuu wa Kampuni ya JATU PLC, Bw Mohamed Simbano amesema uamuzi huo umekuja kufatia Serikali kumteua msanii huyo kuwa Balozi wa Wazara ya Maji hivyo kwa kutambua umuhimu wa Maji hususani katika sekta ya Kilimo.
JATU kwa kutambua uzito na umuhimu wa sekta hiyo tumeamua kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kutangaza na kutoa elimu juu ya miradi mbalimbali ikiwemo kilimo, Ufugaji, Maji, Ujenzi na Utalii.
"Kwetu sisi sekta ya Maji ni Moja ya Nguzo muhimu sana katika kuleta mapinduzi ya Kilimo, hasa kilimo hasa cha Umwagiliaji ambacho tumekua tukifanya katika mikoa mbalimbali ndani ya miaka mitano toka kuasisiwa kwa kampuni kwakweli tuna kila sababu ya kujivunia na kutembea kifua mbele tukiwa kama vijana tuliothubutu kwa kuishi ndoto zetu kwa kufanya kazi kwa vitendo na kisha kuaminiwa na kulelewa na serikali kwa kipindi chote cha miaka mitano" Alisema Bw Simbano.
Alisema JATU PLC pamoja na kupitia changamoto za hapa na pale wamefanikiwa kusajili kampuni katika soko la hisa la DSE, kufungua ofisi kikanda ndani ya nchi na afrika mashariki kwa kuanza na Kenya kwa ajili ya kupanua wigo wa masoko ya ndani na nje, kufungua Kampuni ya Bima ya Kilimo na Ufugaji, pamoja na ongezeko la Wakulima zaidi ya elfu tano.
Bw Simbano alibainisha mafanikio mengine yaliyo patikana katika kipimdi hicho cha miaka mitano kuwa ni pamoja na kutoa ajira rasmi mia tano na zisizo rasmi zaidi ya elfu kumi, kuchochea maendeleo ya Taifa kwa kulipa kodi mbalimbali pamoja na kukuza kipato kwa wanachama wake kwa kufanikiwa kuweka maifumo wezeshi na kuwawezesha kufanya uwekezaji katika kampuni hiyo kwani asilimia 95 inamilikiwa na watanzania.
Kwa upande wake Balozi mteule msanii Mrisho Mpoto alisema sitawangusha na kufanya kazi ya kutoa elimu kwa jamii kutambua umuhimu wa Sekta ya Maji katika shughuli mbalimbali hususani Kilimo, kwani serikali ya wamu ha sita chini ya rais Samia Hassan imeonyesha kuweka mkazo mkubwa katika utekelezaji wa miradi ya sekta ya maji nchini kwa lengo la kumtua mama ndoo kichwani
"Naishukuru Serikali kwa kuniteua kuwa balozi wa Wizara ya Maji, leo JATU mmeniteua kwa mara nyingine kuwa balozi wenu kwa mkataba mkubwa wenye heshima kubwa, nawahidi sitawangusha nitatumia kipindi cha Kaa Hapa awamu ya Pili kupitia Chaneli 10 siku Jumatano Saa nne Usiku,na Marudio yake Jumanne saa tano Usiku ili kutoa elimu kwa watanzania kujua umuhimu wa sekta ya Maji" Alisema Mpoto.
Alisema Serikali katika sekta ya Maji, Mfano fedha za msaada za Uviko 19 serikali imetenga silimia kumi ya fedha hizo ambayo zaidi ya Bilioni katika sekta ya Maji ambapo ndio sekta pekee iliyopewa fedha nyingi, najua watanzania wengi hawajui hilo lakini hiyo ni kazi yangu ya kuelimisha naenda kuifanya.



