MSTAAFU MIZENGO PINDA KUONGOZA KIKAO SEKRETARIETI YA MWALIMU NYERERE FOUNDATION
TAARIFA KWA UMMA
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda ambae pia ni Mwenyekiti wa bodi ya Taasisi ya kumbukumbu ya Mwl. JK Nyerere Jumamosi 26 Februari 2022 anatarajiwa kukutana na kufanya mkutano na Sekretarieti pamoja na wanachama wa Taasisi hiyo utakaofanyika ukumbi wa Msasani Beach Club uliopo Kawe jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hii leo jijini Dar es salaam na katibu Mkuu wa Taasisi hiyo Mh. Simon Rubugu amesema katika mkutano huo kwa siku hiyo kutatanguliwa na kikao kidogo cha bodi hiyo kitakachoongozwa na Waziri Mkuu huyo Mstaafu akiwa ndiye Mwenyekiti wa bodi ikiwajumuisha pia wajumbe wa Sekretarieti ya Taasisi hiyo kabla ya baadae mchana kukutana na wanachama wa Taasisi.
Aidha katibu Mkuu huyo ametumia fursa hiyo kuwaomba wanachama mbalimbali wa Taasisi hiyo kuhudhuria mkutano huo kwa wingi kwakuwa unakwenda kutoa muelekeo wa Taasisi katika nyanja mbalimbali tangu ilipoanzishwa ikiwa na malengo na dira ya Kuendelea kumuenzi kwa vitendo na Uzalendo Baba wa Taifa hayati Mwl.JK Nyerere.
Hiyo ni mara ya Kwanza kwa waziri Mkuu huyo Mstaafu wa awamu ya nne kukutana na wanachama wa Taasisi hiyo mara baada ya kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi wa Taasisi hiyo ya kumbukumbu ya Mwl.JK Nyerere mwaka Jana.
Moshi Said
Afisa Habari na Mawasiliano wa Taasisi ya kumbukumbu ya Mwl. JK Nyerere
22 Februari 2022



