Breaking News

ABDUL NONDO: SERIKALI TOKENI MAFICHONI TUNATAKA KUJUA HATMA YA WATANZANIA WENZETU WALIOPO UKRAINE

Mwenyekiti wa ngome ya vijana wa chama cha ACT Wazalendo, Abdul Nondo ameitak serikali kupitia Wizara ya Mambo ya nje na Balozi zetu, kutoa taarifa juu Watanzania wenzetu waliopo Ukraine.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vyombo vya habari iliyotolewa leo imesema kuwa ngome ya vijana wa ACT wazalendo imekuwa ikifatilia mgororo unaendelea kati Ukraine na Urusi hivyo kuitaka seikali kutoa taarifa juu ya watanzania waishi nchini humo.

"Tunahitaji taarifa za mara kwa mara katika kipindi hiki kutoka Serikalini kupitia Wizara ya mambo ya nje wizara mambo ya nje tz na Balozi zetu juu ya hali ya watanzania wenzetu" Alisema Nomdo.

Tunaposema watanzania ni pamoja na wanafunzi wakitanzania waliokuwa UKRAINE hadi sasa ni wangapi tayari wametoka nchi ya Ukraine aidha wapo Hungari , Poland , Romania au nchi yeyote za mpakani ni wangapi hadi sasa ? 

Ngome ya vijana wa chama cha ACT wazalendo serikali pia ieleze watanzania wangapi hadi sasa wapo njiani wameondoka kuelekea mipaka ya Poland, Hungari , Romania na kwingineko huko ili kurejeshwa nyumbani?

Kwa mujibu wa taarifa hiyo pia ngome ya vijana umeitaka pia serikali kuelezea kwa kina na kutoa taarifa za kila mara juu ya idadi ya watanzania ambao hadi sasa tayari wamesharejea nchini, Na watanzania wangapi hadi sasa bado wapo UKRAINE hawajaondoka?

"Ni vyema serikali hituambie jitahida gani zinaendelea ili kuwaondoa? Maana kumekuwepo na kimya sana, na mmejificha mno  Information is Power na taarifa ni muhimu sana hasa katika hiki kipindi" Alisema Nondo.

Aidha Ngome ya vijana wa ACT wazalendo imeomba pia ufafanuzi kutoka kwa wizara mambo ya nje kufatia taarifa waliyoitoa kwamba kuna Safe Corridor, Safe Passage au humanitarian Corridor imetengenezwa ili Watanzania hasa walio kwama Sumy wapitie Urusi ambapo walipaswa kuondoka tangu tarehe 5 Machi kuelekea Sudzha, eneo la Urusi ambapo watapewa msaada na Jeshi la Urusi kupelekwa Belgorod.

Kumekuwepo na taarifa ambazo tunazipata kwamba wanazuiwa Barabarani na vikosi vya UKRAINE yaani kuna Blockouts barabarani kuzuia sababu hata usafiri walinyimwa, hivyo hawajaondoka na hii sio kwa watanzania tuu hata raia wa nchi zingine kama Nigeria, India, Afika ya kusini na nchi zingine wote wanazuiwa hii Safe Corridor ya Urusi ila kuna nchi kama India imetafuta mbadala.

Alisema taarifa hiyo inaeleza kuwa India imeelekeza Raia wake kupitia Poltava kuelekea Hungari, na Mafisa wa Ubalozi wa India wapo mji wa Poltava ili kuwapokea kuelekea Hungari na wanafunzi wao hivyo kuwarudisha nchini kwao. 

"Serikali kupitia wizara ya Mambo ya nje na Balozi zetu wapo kimya hawajatuambia ni mbadala upi ambao watanzania wenzetu wanapaswa kuchukua ili kuondoka na wanawasaidia namna gani"

Taarifa hiyo iliongeza kuwa Serikali ya India wameipa jina Operation Ganga #OperationGanga na wanaifanya kwa weledi taarifa kila wakati , kuna Uratibu mzuri wao wanajua idadi ya watu wao walio Poland, Hungary, Romania na nchi zingine mpakani .

Serikali ya India inajua Idadi ya watu wao waliokwama Sumy, na muda wote wanatoa taarifa, wao ndio walikuwa ni moja ya nchi yenye raia wengi UKRAINE

"Cha kushanganza Sisi watu wetu sio wengi sana kama wahindi hadi kushindwa kuratibu zoezi hili , tunashindwa toa taarifa , tunashindwa hata kutoa idadi ya waliopo Ukraine hasa Sumy, walio Poland, Romania na nchi zingine mpakani, hakuna taarifa wangapi wamerejea nchini"