Breaking News

LHRC, TEF WAJADILI SHERIA YA MAKOSA YA JINAI, UTAKATISHAJI FEDHA

Afisa Mwandamizi na Uchechemuzi wa LHRC Raymond Kanegene akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo iliyofanyika katika hotel ya Protea courtyard jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile akiongea na waandishi wa habari iliyofanyika katika hotel ya Protea courtyard jijini Dar es salaam
Wahariri wa Star TV Michael Noel akiongea na waandisho wa habari juu ya warsha hiyo iliyofanyika katika hotel ya Protea courtyard jijini Dar es salaam.

Dar es salaam:
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimekutana na wahariri wa vyombo vya habari nchini kujadili Sheria ya Makosa ya Jinai na ya Utakatishaji Fedha zilizopitishwa hivi karibuni na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Afisa Mwandamizi na Uchechemuzi wa LHRC Raymond Kanegene amesema wameamua kujadili sheria hizo na wahariri wa vyombo vya habari kwa sababu wanamsaada mkubwa katika jamii.

“Siku ya leo tumekutana na Wahariri kwa ajili ya kuwafahamisha mambo makubwa ambayo yamepitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni. Kwanza kuna hii sheria ambayo imeletwa kwa muswada Na. 7 kipaumbele chetu hapa ni kwenye Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na Sheria ya pili ni Sheria ya Kudhibiti na Kuzuia Utakatishaji Fedha,” amesema Kanegene.

“Lengo ni kuwajulisha Wahariri kwa sababu wao wanamchango mkubwa katika jamii kwani kuna baadhi ya mazuri na mabaya katika sheria ambayo watasaidia kutaika kuyasemea,” ameongeza.

Amesema kuwa wanatumia fursa hiyo kuwafahamisha mazuri, lakini pia maeneo ambayo bado yanachangamoto  katika Sheria hiyo ya Mwenebdo wa Makosa ya Jinai.

Ametolea mfano katika Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 1985 kwa kusema kuwa Sheria hiyo imerekebishwa kifungu cha 91 ambapo kuna mamlaka ambayo Mwendesha Mashataka amepewa nguvu ya kueweza kumuachia mtu pale ambapo anaona hakuna ushahidi wa kutosha.

“Lakini bahati mbaya ni kwamba kifungu hiki kilikuwa kinatumika katika namna ambayo watu wengi wamekuwa na malalamiko kwani wanaachiwa lakini baada ya dakika kadhaa wanakamatwa tena. Yani kulikuwa hakuna ukomo wa ukamataji,”.

Kwamba kwa mujibu wa Sheria iliyopitishwa na Bunge kwa sasa Mwendesha Mashtaka akitumia kiufungu hicho ndani ya masaa 24 anatakiwa aweze kumfikisha mtuhumiwa mahakamani na awe na ushahidi wa kutosha.

Aidha Kanegene amesema jambo lingine ni suala la kutomshitaki mtu hadi pale upelelezi utakapokamilika kwani kumekuwa kunachangamoto ya watu kushtakiwa huku upelelezi ukiwa haujakamilika, lakini pia hakuna ushahidi wa kutosheleza.

Amesema hali hiyo imekuwa ikifanya watu wasote mahabusu, hivyo uzuri wa kifungu hicho kwa sasa mtu atatakiwa kushtakiwa upelelezi ukiwa umekamilika.

“Ingawa kuna makosa ambayo yamewekwa kwamba hata kama upelelezi haujakamilika mtu anaweza kushtakiwa kwa mfano kosa la uvamizi kwa kutumia silaha na kosa la shambulizi la mwili,” amesema Kanegene.

Hivyo amesema ni vyema kukawa na ukomo wa upelelezi kama ilivyo kwa nchi ya Uganda ambayo wanatumia siku 120 kwa makosa ya Mahakama za chini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile ameipongeza LHRC kwa mkutano huo wenye teja kwa maendeleo ya Taifa letu katika kuhakikisha linakuwa na utawala ulio na misingi mizuri ya sheria.

Amesema kuwa ni vyema kuhakikisha mtu hashatikiwi kama upelelezi haujakamilika, lakini pia ni vyema makosa yote yawe na dhamana kama ilivyo kwa nchi ya Kenya