MFUMUKO WA BEI UMESHUKA MPAKA 3.7
Ofisi ya taifa ya takimu (NBS) imetangaza takwimu za gali ya mfumuko wa bei wa taifa ambapo takwimu zinaonyesha kuwa umepungua hadi Asilimia 3.7 kutoka asilimia 4.0 iliyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi January 2022.
Akizungumza jijini Dar es salaam mkurugenzi wa Takwimu za ndani na sensa ya watu na makazi Bi. Ruth Minja alisema kushuka kwa mfumuko kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi cha Mwaka ulioishia mwezi February 2022.
"Mfumuko wa bei wa taifa umeshuka kutokana na kuwepo na kushuka kwa bei za bidhaa za vyakula na visivyo vya vyakula kwa mwaka ulioishia mwezi February ya mwaka 2022 ukilinganishwa na kipindi cha mwaka ulioishia mwezi January" Alisema Bi. Minja
Amezitaja baadhi ya bidhaa za vyakula ambazo zimeoonyesha kupungua kwa kwa mfumuko wa bei kuwa ni Matunda kutoka asilimia 9.5 hadi 5.2, Mboga mboga kutoka asilimia 5.0 hadi 3.7, kunde asilimia 7.1 hadi 2.6 na Njegere asilimia 6.8 hadi 4.2.
Nyingne ni siagi kutoka asilimia 6.6 hadi asilimia 6.5, Tambi kutoka asilimia 4.2 hadi 3.9, bodhaa zingine za ngano kutoka asilimia 8.4 hadi 5.8,
Aidha Bi Minja aliongeza kuwa kwa ujumla mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka unaoishia mwezi February 2022 umepungua hadi asilimia 6.1 kutoka asilimia 6.3.kwa mwaka ukllioishia mwezi January 2022
Alisema Mfumuko ambao haujumuishi bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi February mwaka ulioishia mwezi January 2022 nao umepungua hadi asilimia 2.7 kutoka asilimia 3.1 iliyouwa mwaka unaoishia mwezi January 2022.



