Breaking News

TAWA YAPOKEA MSAADA WA MAGARI KWA AJILI YA OPERESHENI KATIKA PORI LA AKIBA LA SELOUS

Mkurugenzi Mkazi wa Frankfurt Zoological Society Dkt. Ezekiel Dembe (kushoto) akimkabidhi magari Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Kusini Mashariki kutoka TAWA Abraham Jullu katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkazi wa Frankfurt Zoological Society Dkt. Ezekiel Dembe (kushoto) wakikata utepe na Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Kusini Mashariki kutoka TAWA Abraham Jullu katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es salaam
Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Kusini Mashariki kutoka TAWA Abraham Jullu akionyesha funguo mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Frankfurt Zoological Society Dkt. Ezekiel Dembe katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es salaam
Pichani ni Magari yaliyotolewa msaada na Frankfurt Zoological Society chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) kupitia mradi wa kufuatilia vifo vya Tembo (Mike) katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es salaam

Dar es salaam.
MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imepewa msaada wa magari mawili
yenye thamani ya shilingi milioni 130
chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) kupitia mradi wa kufuatilia vifo vya Tembo (Mike).

Akizungumza katika hafla fupi ya kupokea magari hayo jijini Dar es salaam, Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Kusini Mashariki kutoka TAWA, Kamanda Abraham Jullu alisema msaada wa magari hayo  yatasaidia operesheni za kufuatilia vifo vya Tembo katika Pori la Akiba la Selous.

"Tanawashukuru wadau hawa wa maendeleo kwa kutupa magari haya, naamini magari haya pamoja na kuboresha utendaji wetu pia yatatusaidia sana katika opereshani zetu," Alisema Kamanda Jullu.

Alisema napenda kuwahidi kuwa magari haya tutayatunza  na kuyathamini na kuyatumia kama ilivyopangwa.

Mapema akizungumzia hali ya vitendo vya ujangili wa Tembo nchini kamanda Jullu alisema kwa sasa vitendo hivyo vimepungua kutokana na kuwepo na ushirikiano mkubwa kati yao na wadau.

Nae Mkurugenzi Mkazi wa Frankfurt Zoological Society, Dkt. Ezekiel Dembe alisema wametoanmsaada huo wa  magari kwa ajili ya kusaidia ufanyaji wa operesheni katika Pori la Akiba la Selous.

Alisema TAWA kwa kipindi kirefu wamekuwa ni washirika wao, hivyo ndiyo maana wameamua kutoa msaada wa magari hayo kutoka Umoja wa Ulaya.

Mkurugenzi Mkazi wa Frankfurt Zoological Society Dkt. Ezekiel Dembe na Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Kusini Mashariki kutoka TAWA Abraham Jullu wakiwa kaika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es salaam.