WATATU MBARONI WAKUTWA NA MENO YA TEMBO 25 JIJINI DAR
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limewakamata watu 3 wakiwa na vipande 25 vya meno ya tembo vyenye uzito wa Kg 20.9
Akizungumza jijini Dar es salaam kamanda wa kanda maalim ASP Jumanne Murilo amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kufatia oparation maalum ya kuzuia uhalifu iliyofanyika kuanzaia Feb 25 hadi March 9 mwaka huu.
Alisema katika oparationi hiyo jeshi la polisi kwa kushirikiana na limefanikiwa Kikosi Kazi cha Kuzuia na kupambana Ujangili katika eneo la Ubungo NHC Dar es salaam walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na vipande 25 vya meno ya tembo vyenye uzito wa Kg 20.9.
Kamanda Murilo alisema katika uchunguzi wa awali uliofanywa na jeshi hilo umebaini meno hayo ni sawa na Tembo 14 walio uawa yalikutwa yakiwa yamefichwa katika moja ya nyumba ya mtuhumiwa hao ambapo pia ilikutwa gari yenye namba ya usajili T. 818 DCA Toyota Wiills iliyotumika kusafirisha hayo.
Amewataja watuhumiwa kuwa Gabriel Mgana, mkazi wa Ubungo NHC 2, Haffarman Yona maarufu kama Mnyaturu mkazi wa Kinyerezi na Felician Cyril mwenye umri wa miaka 57, Mnyaturu mkazi wa Kinyerezi jijini Dar es salaam.
"Jeshi la polisi linaendelea kufanya Uchunguzi wa kina kujua Tembo waliouawa ni wa eneo lipi na thamani ya meno hayo ni kiasi gani na yalikuwa yanatarajiwa kupelekwa au kuuzwa wapi" Alisema Kamanda Murilo.
Aidha pia jeshi la Polisi katika operesheni hiyo pia limefanikiwa kuwakamata Khatib Abdala Msambaab(33) mkazi wa Banana Kitunda, na wenzake 3 kwa tuhuma za wizi kwa njia ya mtandao katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam.
Alisema mara baada ya kukamatwa watuhumuwa hao ulifanyika Upekuzi wa kina katika nyumba za watuhumiwa hao na walikutwa na jumla ya kadi (line) za simu 46 za kampuni tofauti tofauti, Vizibao 4 vya uwakala
"Kumekuwepo na matukio ya wizi kwa njia ya mtandao nchi katika oporasheni hiyo watuhumiwa walikutwa na kadi (line) za simu 46 za makampuni mbalimbali ambazo wamekuwa wakizitumia kufanyia uhalifu ikiwepo kujifanya wanatoa huduma za kusajili kadi pamoja na huduma zingine ambazo utolewa na makampuni ya simu" Alisema



