Breaking News

TBS YATOA ELIMU KWA WAHARIRI KUHUSU UTENDAJI WAKE

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bi.Viola Masako akifungua mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari uliyofanyika makao makuu ya TBS Ubungo jijini Dar es salaam.
Meneja Viwango shirika la viwango TBS Yona Afrika akifafanua jambo katika mkutano na Wahariri wa vyombo vya habari kuhusu umuhimu wa ushiriki katika mchakato wa uandaaji viwango.

Dar es Salaam
Shirika la Viwango Tanzania TBS limetoa wito kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini kutumia kalamu zao vizuri katika kufikisha habari zilizo sahihi katika jamii.

Akizungumza na wahariri hao leo Machi 21, 2022 katika Ofisi za TBS Makao makuu Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS Viola Masako amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kumuelimisha wahariri juu majukumu ya TBS na kazi zake ili atumie kalamu kuelimisha jamii.

“Kwa kuwaelimisha wahariri shughuli mbalimbali zinazofanya na shirika la TBS rkwani wahariri ndo jicho la taifa, mtakachokwenda kuongea, mtakacho elimisha jamii ndicho kitakachopokelewa, ” Amesema Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bi. Viola

Aidha mada mbalimbali zilitolewa ikiwemo umuhimu wa ushiriki katika mchakato wa uandaaji viwango, Huduma zitolewazo na kuruhenzi ya upimaji na Ugezi.