Breaking News

FURAHIA EDUCATION YAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA, KUTOA ELIMU BURE

 

Taasisi za umma na binafsi zimeombwa kuunga mkono jitihadi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na rais Samia Suluhu Hassan hususani katika jitahda zake zqa kuhakikisha kila mtoto anapata elimu.

Akizungumza jijini Dar es salaam mafanikio ya mwaka mmoja tangu kungia madarakani rais Samia mkuu wa chuo cha FURAHIKA, Bw. David Msuya alisema selikali  imeonyesha kuwa na dhamira ya dhati ya kuhakikisha kuwa inawaletea maendeleo wanachi katika nyanja mbalimbali ikiwepo elimu.

Alisema kwa kutambua jitihada hizo serikali wao kama wadau wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na serikali kupitia mradi wa kuwasaidia wale ambao awakupata matokeo mazuri shuleni kupata nafasi ya kijiendeleza na kupata ujuzi ambao utawawezesha kujiajili na kuajiliwa katika sekta mbalimbali.

"Katika kuhakikisha kila kijana anapata elimu chuo chetu kimekuwa kikitoa elimu bure kwa vijana ambao awakufanikiwa kupata matokeo mazuri kwa kuwapatia ujuzi katika kozi za mda mfupi mbalimbali ambazo zitawasaidia kuajiliwa au kujiajili" Alisema Bw. Msuya

Alisema mafunzo ambayo yamekuwa yamekuwa msaada kwa wahitimu kwa kuwawezesha kuajiliwa pamoja na akujiajili wenyewe hivyo kusaidia jitihada za serikali za kuhakikisha inawapaitia elimu vijana nchini.

Ametaza program ambazo zinafundishwa chuoni hapo ni Ushonaji, Tehama, Ufundi wa Magari, Umeme wa majumbani, secretary pia chuo kimekuwa na ratiba ya masomo ya jioni kwa wale ambao wameajiliwa.

Chuo kinampongeza rais Samia kwa namna ambavyo amekuwa akiongoza na jitihada ambazo amekuwa akizichukua kutatua changamoto mbalimbali husasani elimu kwa kuweka mazingira mazuri kwa watoto kuweza kupata elimu.

"Nitoe wito kwa jamii, wazazi, walezi na wadau kuunga mkono jitihada ambazo serikali imekuwa akizichukua za kuhakikisha kuwa inaweka mazingira wezeshi kwa lengo la kusaidia watoto kupata elimu nchini"