Breaking News

WAZIRI MAKABA: SERIKALI INAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI

Na Timothy Marko
Serikali imesema itaendelea kushirikiana kampuni ya usambazaji mafuta ya Total Energies ili kuboresha sekta hiyo ya mafuta hapa nchini.

Akizungumza katika uzinduzi  wa nembo mpya ya kampuni hiyo jijini Dar es salaam waziri wa nishati, Mhe January Makamba amesema itaendelea kushirikiana na kampuni katika kujenga miundombinu ikiwemo ujenzi wa kituo kikuu cha usambazaji mafuta hapa nchini.

‘”Mahitaji yamafuta yameongezeka hasa kipindi cha janga la uviko 19 na kusabsbisha bei ya mafuta kuongezeka kutokana wimbi hili, serikali katika bunge lijalo tutajadili jinsigani kutatua suala hili la upandaji mafuta”.Amesema  Waziri Makamba.
Aidha ameongeza kuwa bei za mafuta zitazidi kupanda kutokana na vita vya Ukraine hivyo serikali itangalia namna ya upatikanaji wa nishati ya mafuta hapa nchini.

Amesema  serikali inaipongeza kampuni hiyo kuzindua kituo cha solar ili kukabiliana na upungufu wa nishati katika sekta  nishati hapa nchini.
‘Tunawapongeza Total kuzindua kituo cha solar total nimdau wa uchumi wa maendeleoya nchi yetu”. Ameongeza waziri Makamba.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa kampuni ya Total Energies, Jean Francois schoepp amesema  lengo la kampuni hiyo nchini nikuonesha mabadiliko na kuchochea sekta ya nishati hapa nchini