JUMIKITA: WAANDISHI WA HABARI MITANDAO YA KIJAMII JITOKEZENI KWA WINGI KUSHIRIKI SEMINA YA TCRA
Katibu wa JUMIKITA, Bi. Catherine Ngowo ambaye pia ni mmiliki wa mtandao wa Carry Mastory akielezea namna ambavyo waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari vya mtandaoni watavyo nufaika na semina iliyoandaliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa JUMIKITA, Bwana Shabani Omar akifafanua jambo kuhusu ushiriki wa waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari vya mtandaoni katika semina iliyoandaliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini Dar es salaam.
Dar es Salaam:
Jukwaa la Waandishi wa Habari wa Mitandao ya Kijamiia Tanzania (JUMIKITA) limetoa wito kwa wadau na wamiliki wa vyombo vya habari vya mtandaoni kushiriki katika Semina iliyoandaliwa kwa ajili yao na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa ushirikiano na Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA).
Akizungumza jijini Dar es salaam Katibu wa JUMIKITA, Bi. Catherine Ngowo amesema lengo la semina hiyo itakayofanyika tarehe 18 na 19 Mei ni kuwajengea uwezo pamoja na kujadiliana juu changamoto mbalimbali wanazokutana nazo
“JUMIKITA imepokea mwaliko huu rasmi wa wito kwa wadau wote kujitokesha kwa wingi kushiriki semina hiyo muhimu ambapo washiriki wote watatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kupotia link ambayo inapatikana katika website ya TCRA au kujiandikisha ofisi za JUMIKITA" Alisema Bi. Ngowo
Alisema hii ni moja ya fusra kubwa kwa wadau hivyo nitoe rai jitikezeni kwa wingi kushiriki semina hii kwani kwa sasa tunatambulika, na moja ya sehemu sahihi za kueleza changamoto tunazokutana nazo kwa Serikali ili zipatiwe ufumbuzi.
Mapema akizungumzia semina hiyo mwenyekiti wa JUMIKITA, Bw. Shabani Omar ametaka wadau wamiliki wa vyombo vya habari vya mtandaoni wote kuwa wamoja.
“Nitoe wito kwa wadau na wamiliki wa vyombo vya habari vya mtandaoni wote tuungane pamoja tuna sababu ya msingi ya kuwa wamoja kwani kwa kufanya hivyo itasaidia sana katika utatuzi wa changamoto zetu,” Alisema Bw. Omar
Alisema Jukwaa hilo tayali walishakaa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) na kukubaliwa kuundwa kwa jukwaa hilo ambalo litaunganisha wadau na wamiliki wote wa vyombo vya habari vya mtandaoni.





