SAKATA LA WAPI ALIPO ASKOFU MKUMBO (MZEE WA YESU) UAMIAJI WATOA KAULI NZITO
Kufuatia taarifa za kudaiwa kukamatwa kwa Askofu Mukombo Muyondi au Mulilege Mkombo Muyondi Kameka (Mzee wa Yesu) na maafisa wa uhamiaji, Jeshi hilo lmetoa taarifa kuwa mtu huyo amekuwa akiishi Nchini kinyume na sheria za Nchi.
Akizungumzia suala hilo ambalo limelipotiwa kwenye vyanzo vya habari vya kuaminika, Msemaji wa Uhamiaji, Paul Mselle amesema kuwa Askofu Mukombo Muyondi au Mulilege Mkombo Muyondi Kameka amefukuzwa Nchini ikidaiwa kuwa ni raia wa Congo ambaye anaishi Nchini kinyume na taratibu, ambapo imeelezwa kuwa jambo hilo limefanikishwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Ubalozi wa Congo nchini
"Mara ya kwanza Mtuhumiwa aliondoshwa nchini mnamo Februari 02, 2011, mara ya pili Agosti 28, 2019 na sasa leo Mei 24, 2022 baada ya kubainika yupo tena nchini mnamo Mei 15,2022" amesema Msemaji wa Uhamiaji, Paul Mselle
Amesema kuwa Askofu Mulilega huyo anarejeshwa nchini kwao kwa mujibu wa kifungu na 25 (2) (c)cha sheria ya uhamiaji sura ya 54 ya mwaka 2016.
Aidha Mselle amewataka Wananchi kutompokea kwenye familia, nyumba za ibada na kutoshirikiana nae kwa namna yoyote ile na atakayefanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Itakumbukwa hivi karibuni Mke wa Askofu Mkumbo alijitokeza kwenye vyombo vya habari na kueleza namna Mme wake alivyochukuliwa na kupelekwa kusikojulikana, huku msemaji wa kwa niaba ya waumini wa kanisa lake lililopo Boko, Dar es Salaam waiiomba Serikali kuingilia kati suala hilo baada ya kudai kuwa walimtafuta baada ya kuchukuliwa lakini hawakujua alipopelekwa, ikiwa ni baada ya kudai walimtafuta kwenye vituo vya mbalimbali vya polisi Jijini Dar es Salaam.
Lakini msemaji huyo alieleza kuwa endapo Askofu huyo angekuwa anakabiliwa na tuhuma yoyote kama ilivyodaiwa kuwa anakabiliwa na tuhuma ya Uraia kutokana na maelezo yaliyodaiwa kutolewa na maafisa wanodaiwa kumkamata Jumapili usiku Mei,15 2022 wagemchukulia hatua za kisheria kuliko mazingira yaliyotumika.




