Breaking News

TIRA YAZITOZA FAINI KAMPUNI NNE ZA BIMA KWA KUKIUKA MWENENDO WA ULIPAJI MADAI, FAIDA KWA WATEJA

Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA), Dkt. Baghayo Saqware akifafanua jambo kwa wanahabari wakati akitoa taarifa kuhusu hatua zilizochukuliwa na mamlaka ya hiyo kwa kampuni nne za bima zilizokiuka mwenendo sahihi wa ulipaji madai na fidia kwa wateja jijini Dar es salaam.
Meneja wa Utekelezaji Sheria na Kushughulikia malalamiko, Bwana Okoka Mgavilenzi akielezea namna kampuni hizo zilivyokiuka masharti ya Bima jijini Dar es salaahi
 

Dar es Saalam:

Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA), Dkt. Baghayo Saqware amewataka watanzania kuendelea kutumia huduma za bima nchini na kutosita kupeleka Malalamiko yao kwa Kamishna wa Bima pindi wanapoona kampuni za bima haziwatendei haki.

Akizungumza jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa kuhusu hatua zilizochukuliwa na mamlaka ya usimamzi wa bima kwa kampuni nne za bima nchini zilizokiuka mwenendo sahihi wa ulipaji madai na fidia kwa wateja.

Dkt Saqware amesema kampuni hizo ni pamoja na Kampuni ya Insurance Group of Tanzania (IGT), Kampuni ya Jubilee, Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Bima ya UAP ambapo zimekiuka kifungu 131(1)(2)(4) cha sheria ya Bima Na. 10 ya mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake.

Amesema kwa nyakati tofauti kuanzia tarehe 01/10/2021 - 15/02/2022 Kamishna wa Bima amepokea malalamiko zaidi ya 48 dhidi ya kampuni ya Insurance Group of Tanzania (IGT) ambapo Lalamiko moja moja lilihusiana na kiwango kidogo cha fidia kilichotolewa kwa munufaika wa bima, Malalamiko nane ni kuhusu ucheleweshaji wa mchakato wa madai na Malalamiko matatu yanahusisha kutakaa madai bila kuwa na msingi wa kuyakataa.

"Mamlaka imebaini kuwa kampuni hii, imeanzisha upya uchunguzi wa baadhi ya malalamiko ambayo awali wayakubali na kutoa Hati ya Kukubali kulipa fidia, jambo ambalo linaleta dukuduku na wasiwasi wa mwenendo wa wataalam na nia ya utoaji haki kwa wateja"Alisema Dkt Saqware.

Aidha Mamlaka imezitoza faini ya kiasi cha Tsh 5,000,000.00 kwa Mwenyekiti wa Bodi ya IGT kwa kutoishauri na kutosimamia vyema Menejimenti ya kampuni hivyo kusababisha wateja na wananchi kukosa haki zao.

Akitolea ufafanuzi kuhusu Kampuni ya Jubilee Dkt Saqware amesema Kwa nyakati tofauti kuanzia tarehe 01/10/2021 - 06/05/2022 Ofisi ya Kamishna wa Bima imekuwa akipokea malalamiko zaidi ya 04 dhidi ya kampuni hii.

"Kwa kuzingatia Sheria na taratibu za uendeshaji wa Biashara za Bima nchini, Mamlaka inachukua hatua nne ya kuiagiza Kampuni ya Jubilee kulipa kiasi chote cha 511,065.49 Euro kwa Wizara ya Maji kama ilivyoagizwa 9 katika kikao cha tarehe 18. Novemba 2022 ndani ya siku 14 kuanzia siku ya tangazo hili" Aliongeza Dkt Saqware.

Dkt Saqware aliongeza kuwa Kampuni ya Bima ya Resolution Dkt Saqware amesema katika nyakati tofauti imekuwa ikikagua na kushauri namna nzuri ya uendeshaji wa kampuni hii baada ya kuona uwezo wake wa kifedha unazorota kutokana na usimamizi mbovu, mienendo yasiyo ya kitaalamu na ukiukwaji mkubwa wa sheria na ufanyaji wa biashara ya bima ulifanywa na Wakurugenzi na Afisa Mkuu wa kampuni hii

Alisema TIRA Inatoa adhabu ya kiasi cha Tsh 5,000,000.00 kwa Wakurugenzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hii kwa kila kosa la kutofuata taratibu za kibima hivyo kuchafua taswira ya soko la bima.

Akizungumzia Kampuni ya Bima ya UAP Dkt Saqware alibainisha kuwa katika nyakati tofauti kuanzia tarehe 01/10/2021 - 06/05/2022 Kamishna wa Bima amekuwa akipokea malalamiko zaidi ya 04 dhidi ya kampuni hiyo hivyo ameiagiza kampuni hiyo kulipa fidia mara ndani ya siku 7 kuanzia tarehe ya taarifa.

Nae Meneja wa Utekelezaji Sheria na Kushughulikia malalamiko Bwana Okoka Mgavilenzi amesema katika Biashara ya Bima Kampuni zinaongozwa na uaminifu kwa kuwa wanashughulikia vitu vinavyogusa maisha ya watu.

Alisema moja ya wajibu wa TIRA ni kuwalinda watumiaji wa bima yaani wananchi na kuendeleza soko, imetoa onyo kwa kampuni za bima nchini zitakazochelewesha ama kuchezea haki ya fidia ya mwananchi.