BENKI ABSA YAJA NA MPANGO WA KUWAINUA WAJASILIMALI WADOGO NA KATI
Timothy Marko
Katika kuhakikisha sekta kifedha inakuwa Benki ya ABSA kwa kushirikiana Benki kuu imeanzisha Mpango wa kuwainua wajasiliamali wadogo na kati kwa lengo la kusaidia ukuaji wa uchumi jumuishi.
Akizungumza katika Uzinduzi wa Mpango Mkuu wa kitengo Cha Biashara wa Benki hiyo, Bwana Absa Melvin Saprapasen amesema lengo la mpango huo ni kuwasaidia wafanyabishara hao wadogo wasio katika mifumo isiyo rasmi na kuwapa ujuzi.
"Lengo la benki yetu kupitia mpango huu ni kuwawezesha na kuwakuza wafanyabishara hao wadogo kuwaweza kuwa wafanyabishara wa kubwa". Alisema Bw. Melvin.
Bw. Melvin Alisema ukuzaji wa wafanyabishara wadogo wadogo unaendana sambamba ukuzaji wa Sekta kilimo unaoendana kukuza thamani ya Mazao.
Alisema Asilimia 40 ya pato la taifa inachangiwa na sekta ya Biashara ndogondouchumi.
"ABSa tunalenga kuwa sapoti katika Teknojia ya Tehama licha ya kukabiliwaa na changamoto ya uelewa mdogo wa Elimu ya fedha". Aliongeza Melvin.
Naye Mkurugenzi wa taasisi za Mabenki nchini kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bwana Nyoni kenedy amesema Serikali ya awamu ya sita inathamini mchango wa wafanyaBiashara wadogo na kati katika kujenga uchumi





