EFM YAWATAMBULISHA DINA MARIOUS, OSCAR OSCAR, WAJA NA KIPINDI KIPYA "JIONI YA LEO"
Mtangazaji wa kipindi kipya cha Jioni ya Leo Dina Marious akizingumza katika hafla ya uzinduzi wa kipindi hicho kipya cha Jioni ya leo kitakacho kuwa kinaruka hewani kuanzia Juamtatu ya tarehe 20 kila siku kuanzia sa 10 jioni mpaka sa 1 usiku kupitia EFM radio.
Mkurugenzi wa Vipindi EFM Bwana Dickson Ponera akifafanua jambo katika hafla ya kutambulisha ujio mpya wa Dina Marious na Oscar Oscar kupitia kipindi kipya cha Jioni ya leo kitakacho kuwa kinaruka hewani kuanzia Juamtatu ya tarehe 20 kila siku kuanzia sa 10 jioni mpaka sa 1 usiku kupitia EFM radio
Dar es salaam:
Mtangazaji maarufu nchini Dina Marious na mchambuzi wa soka Oscar Oscar wametanganzwa rasmi kuja na kipindi kipya cha JIONI YA LEO ambacho awali kilikuwa kikijulikana kama UBAONI kitakachakuwa kikiruka hewani kila siku kuanzia saa 10 jioni kupitia radio ya EFM.
Akizungumza katika hafla ya utambulisha wa kipindi hicho kipya pamoja na watangaji hao iliyofanyika Makao Makuu ya EFM na TVE Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Vipindi wa EFM bwana Dickson Ponera akielezea kuhusu kipindi hicho amesema
Ikumbukwe kuwa awali Dina Marious alikuwa akitangaza kipindi cha Uhondo huku Oscar Oscar akiwa ni mchambuzi wa kipindi cha michezo cha Sports HQ.
Aidha Ponera alisema kipindi hicho kitakuwa kikirushwa kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa 1:00 usiku.
Alimewataja watangazaji wengine ambao sambamba wataungana nao katika kipindi hicho na Roman Shirima, Mpoki na Veronica Frank ambao hapo awali walikuwa wakitangaza kipindi cha UBAONI.







