DC GODWIN GONDWE: SERIKALI ITAENDELEA KUSIMAMIA HAKI ZA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Godwin Gondwe akiwa na moja ya watoto walioshiriki katika tamasha liloandaliwa na kijiji cha makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam.
Dar es salaam:
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Godwin Gondwe amesema Serikali itaendelea kutunga sheria na sera ambazo zitasaidia kusimamia haki za watoto hususani wenye mahitaji Maalum.
Akizungumza katika Tamasha ” lililowakutanisha watoto kutoka maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam wenye ulemavu na walio na mahitaji maalum lililoandaliwa na kijiji cha makumbusho.
DC Gondwe alisema Wilaya ya Kinondoni tumekuwa ikichukua hatua za makusudi ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa makundi Maalum katika kuwawezesha kiuchumi ili waweze kuendesha maisha yao.
“Serikali imekuwa ikitoa fedha kila mwaka kwa ajili ya kuwawezesha wanawake, vijana pamoja na watu wenye mahitaji Maalum ili waweze kujikomboa kiuchumi. Mfano kwa mwaka 2022 tumetoa zaidi ya shilingi milioni 255 zote hizi ni juhudi za Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi wake wanapatiwa huduma bora kwa usawa bila kujali umri, Jinsia au maumbile,” Alisema DC Gondwe.
Alisema pamoja na mambo Mengi mazuri ambayo wanayafanya kwa watu wenye mahitaji Maalum bado kuna changamoto ambazo familia pamoja na watu wenye mahitaji Maalum wanazipitia.
Amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na hali duni za maisha ya familia zenye watoto wenye mahitaji Maalum na hivyo wengine kupelekea kuingizwa kwenye biashara za kuomba omba.
Aidha DC Gondwe ametoa wito kwa waoe wote wanaofanya ukatili wa namna yoyote ile kwa watoto hao kucha mara moja kwani sheria zipo watashughulikiwa kwa sheria.
Mapema Afisa Elimu Makumbusho ya Taifa, Wilhelmina Joseph alisema tamasha hilo limejukuisha watoto wenye mahitaji Maalum wakiwemo wenye uoni hafifi, walemavu wa ngozi na wengine wenye mahitaji Maalum.
“Lengo la tamasha hili ni kuwaweka pamoja na kuweza kushirikiana na kuwajumuisha pamoja wenye mahitaji Maalum na wasio na mahitaji Maalum ili kuonesha kuwa wote wanahaki sawa,” Alisema Wilhelmina.
Tamasha hilo limebeba kauli mbiu ya “Haki sawa kwa wote" limewakutanisha watoto kutoka katika shule za Jeshi la Wokovu, Mgabe, Uhuru Mchanganyiko, Sinza, Shule Msingi Makumbusho na Mikocheni.









