Breaking News

MCHUMI WALTER NGUMA AICHAMBUA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2022 / 2023

Mtalamu wa Masuala ya Uchumi nchini Walter Nguma amesema Ni vyema Serikali kufanyia Marejeo ya Deni la taifa na kufanya marejesho ya fedha za Deni Hilo kuwekezwa kwenye Miradi ya Maendeleo ikiwemo SGR ili kuondana na taifa kuweza kupata Hasara.

Akizungumza wakati akichambua bajeti kuu ya serikali ya mwaka 2022/ 23 jijini Dar es Salaam bwana Walter Nguma amesema Hatua ya Rais mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kutembelea nchi mbalimbali kuwahamasisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini ni hatua nzuri ambayo itasaidia kutachochea ukuaaji wa uchumi.

"Miradi ya kimkakati ni vyema ikamilike kwa wakati itachochea ukuaaji wa uchumi". Alisema Bw. Nguma.

Alisema Hadi Sasa Mradi wa Reli ya kisiasa (SGR) imekamilika kwa Asilimia 98 huku Bwawa la Mwalimu Nyerere limefikia 55, na kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unakuwa na tija kwa kudhibiti upotevu wa Mapato ya Serikali.

Akizungumzia sekta ya elimu Bw. Nguma amesema ni vyema Sekta ya Elimu ifanyiwe Maboresho hasa mitaala ianze kuboreshwa katika vyuo vya walimu ili iendane  na Hali ya Soko la Ajira katika Dunia.

“kidato cha tano na sita wanataraji kuanza kupata Elimu bure. Hivyo Serikali kupitia Wizara ya Fedha itenge fungu kwa ajili ya kuboresha na kuangalia namna gani inaweza kuboresha mtaala yetu,” Alisema Bw. Nguma. 

Na kuhusu uchumi amebainisha kuwa utaratibu wa ukusanyaji mapato umekuwa ni mzuri na rafiki katika ukuaji wa Sekta binafsi huvyo ameishauri Serikali kuendelea kuboresha mifumo ya ukusanyaji mapato ambavyo ni rafiki kwa ukuaji wa Sekta binafsi na kuongeza mapato ya Serikali.

"Wakati uchumi wa Dunia yetu  ukipitia Changamoto za Uviko 19 na Vita vya Ukraine takwimu zimeonesha Uchumi wetu imeshuka kutoka  Asilimia 7 Hadi kufikikia Asilimia 4.5  lakini umeongezeka kutoka Asilimia 4.5 Hadi kufikia Asilimia 4.9'". Aliongeza Nguma.

Nguma Aliongeza kuwa Ni vyema Serikali iongeze nguvu katika huduma za Afya katika hospitali za Wilaya hasa huduma Za Cityscan zipatikane katika Hospital za wilaya  Kama vile Kcmc ..

"Nivyema Serikali ikapunguza Warsha naMikutano nakuwekeza mafunzo kwa Watumishi Vijana kuliko Watumishi wanaoelekea kustaafu". Alisisitiza Nguma.