Breaking News

JESHI LA POLISI LAWATAKA WAMILIKI WA SILAHA KISHERIA KUZISAJILI

Na Timothy Marko
Jeshi la polisi Kanda Maaluum ya Dar es Salaam limewataka wamiliki wa Silaha kisheria kujitokeza katika ofisi za wilaya za kipolisi kuweza kupata mafunzo ya utumiaji wa Silaha na Miiko ya utumiaji wa Silaha hizo.

Akizungumza na waandishi wa Habari  jijini Dar es Salaam kamanda wa Kanda Maaluum ya Dar es Salaam Cp Murilo Jumanne Murilo amesema mafunzo hayo yanalenga kutumia Silaha kwa weledi ambapo mafunzo yanajumuhisha Wananchi waliopata mafunzo ya kijeshi na wasio pata Mafunzo ya kijeshi.

"Wamiliki wa Silaha hizi wanapaswa kujiandikisha kwa OCD wa wilaya, Ambapo Malipo kwa mtandao wa Vodacom". Alisema kamishina Murilo 

Kamishina Murilo Alisema Mafunzo haya yalianza Mwaka 2013 ili wawezekupata kutunza kwa Silaha kwa weledi.

"Silaha sio zakuoneshana asiye tekeleza wajibu huu nikosa la kisheria". Aliongeza Murilo.

Naye, Afisa  Mnadhimu wa polisi ambaye niMkurugenzi uzalishaji Mali wa jeshi Hilo, Betus Silas amesema mafunzo hayo nipamoja nakutunza bunduki na kutumia Silaha.