Breaking News

KILELE CHA SIKU YA HEDHI SALAMA TAASISI YA BINTI SHUPAVU YATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE SHULE YA MSINGI MSASANI ‘A’

Mwenyekiti wa Taasisi ya Binti Shupavu, Hadija Seif akifafanua jambo katika kilele cha siku ya hedhi salama mara baada ya kukabidhi msaada taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya msingi Msasani A iliyopo wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam.
Afisa Ustawi wa Jamii wa Kata ya Msasani wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Msasani A wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam (aliyevaa nguo ya njano).
Bondia wa Kimataifa wa Tanzania ambaye pia ni moja ya waratibu wa tukio hilo, bw. Selemani Kidunda akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Msasani A iliyopo wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam.
Bondia wa Kimataifa wa Tanzania ambaye pia ni moja ya waratibu wa tukio hilo, bw. Selemani Kidunda akigawa taulo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Msasani A iliyopo wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam.


Dar es Salaam:
Taasisi ya Binti Shupavu katika kuadhimisha cha siku ya hedhi salama wametoa msaada wa taulo za kike pamoja sambamba na elimu ya hedhi salama kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Msasani ‘A’ jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Bi. Hadija Seif amesema lengo la kutoa elimu hiyo ni kuwasaidia mabinti kuwa shupavu na kupinga vishawishi ambavyo vitawafanya kutotimiza ndoto zao.

“Kwanini Binti Shupavu, lengo ni kuona mabinti wanakuwa shupavu na kusimama wenyewe na kupinga vishawishi, tunaangalia wasichana ambao wanapata vishawishi na kukatiza ndoto zao,” Alisema Bi. Hadija

Alisema lengo la kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi hao kuwa huru kumweleza mzazi/mlezi wa kiume wanapokuwa katika kipindi cha hedhi ili waweze kupata huduma stahiki ikiwemo kununuliwa taulo za kike.

“Mabinti unatakiwa kujenga urafiki na ndugu zako wa damu, kama vile baba, mama, mjomba, bibi, shangazi, sio watu wengine kama boda boda ambao watawaingiza katika vishawishi hatarishi,” Alisema Bi. Hadija.

Kwa upande wake Mmoja ya wafadhiri wa tukio hilo, Selemani Kidunda amesema Binti Shupavu ni yule ambaye anajiamini na mwenye uwezo wa kuepuka vishawishi hatarishi.

Nitoe rai kwenu watoto wa kike tambueni kwamba hedhi sio ugonjwa na unapokuwa katika kipindi cha hedhi wasiogope kuwaambiwa wazazi wa walezi wako yaani baba na mama.

“Tambueni kuwa Baba ni kama mama usiogope kumwambia, ukipata tatizo mshirikishe na mweleze ili akusaidie,” Alisema Kidunda.

Naye Afisa Ustawi wa Jamii Kata ya Msasani wilayani Kinondoni Mkoani Dar es Salaam, Bi. Kichiki Njovu
 ametoa wito kwa watoto wa kike wanapokuwa na tatitizo kutomweleza kila mtu badala yake wawashirikishe wazazi, walezi au waalimu kwa msaada zaidi.

“Usimwombe msaada mtu yeyote barabarani mfano bodadoda kwani hata kupa msaada bure. Mwisho wa siku badala ya kutatua tatizo utaongeza lingine mfano ujauzito hivyo kushindwa kutimiza ndoto zako kwani hedhi ni chanzo cha kupata ujauzito,” Alisema

Bi Njovu aliongeza kuwa ukikutana na mwanaume utapata ujauzito, ukipata ujauzito nani atakutunza, unakuta wazazi wengine ni wakali wanakufukuza nitoe rai kwenu mjitunze msikimbilie kupata mimba za utotoni.