Breaking News

MAGEREZA : JAMII KUJITOKEZENI KUTOA MISAADA KWA WAFUNGWA

Na Timothy Marko
Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam limewataka wanajamii kutembelea Magereza ilikuweza kutoa Misada Mbalimbali yakijamii ikiwemo taulo za kike kwa Wanawake.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Magereza Mkoa Dar es Salaam ACP George Wambura amesema kuna Changamoto ya upatikanaji wa taulo za kike kwa Wanawake ambao ni wafungwa.

"Sambamba na Hilo kumekuwa na Changamoto ya wa huduma za Matibabu,Mfungwa ni Mwanajamii Kama wengine  wanajitaji mahitaji Mbalimbali". Alisema ACP Wambura.

ACP Wambura Alisema Mfungwa ni Mwanajamii aliyehukumiwa kwa Mujibu wa Sheria lakini anahaki za kupata mahitaji Muhimu Kama wanajamii wengine.

Alisema utaratibu wa kutoa Misaada hiyo ni lazima uandike Barua juu ya kuleta mahitaji hayo.

"Magereza ni sehemu Salama ambapo wafungwa wanajifunza kilimo ili kumwezesha anapotoka gerezani kuwa na stadi za maisha'' Aliongeza ACP Wambura.

Wambura Alisisitiza kuwa kume kuwa na changamoto za Mavazi hasa Kwa Madada poa pindi wanapoingia Magerezani.