PROF. LIPUMBA AICHAMBUA BAJETI KUU YA SERIKALI MWAKA 2022/23..ABAINISHA MAPUNGUFU NA KUTOA USHAURI
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba ameainisha mapungufu ambayo yanakabili mchakato wa kujadili bajeti kuu ya Serikali kwa sasa ikilinganishwa na ilivyokuwa kipindi cha nyuma.
Akizungumza makao makuu ya vhama hicho buguruni jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha uchambuzi wa makadirio na mapendekezo ya bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka 2022/2023 iliyowasilishwa bungeni hivi karibuni na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba.
Ameeleza kuwa utaratibu wa zamani wa kajadili bajeti ulianza kwa kusomwa hotuba ya hali ya uchumi wa Taifa asubuhi ukifuatiwa na kusomwa kwa mapendekezo ya bajeti jioni.
“Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa na Vitabu vya Bajeti vyenye mafungu ya matumizi viligawiwa kwa Wabunge. Serikali ilikubaliana na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kuwa vitabu hivyo vitawekwa kwenye tovuti ya Wizara ya Fedha ili wananchi na wadau wa bajeti waweze kupata taarifa,” amesema Prof. Lipumba.
Amebainisha kuwa katika Awamu ya Nne, iliamuliwa kwamba Hotuba ya Bajeti isianze bali iwe ya mwisho baada ya kujadili Bajeti za Idara na Wizara za Serikali huku Wabunge wakiwa hawapewi Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa.
“Miaka ya 1960 na 1970, wakati Kitabu hiki kinachapishwa kwa kiingereza kilikuwa na jina la Economic Survey: Background of the Budget. Uchambuzi wa Hali ya Uchumi ndiyo unaiongoza Serikali katika kuandaa bajeti inayowasilishwa Bungeni,” amefafanua Prof. Lipumba
“Ili Wabunge wajadili vizuri Bajeti wanahitaji kuwa na kitabu kinachochambua maendeleo ya Uchumi ya Sekta zote, kilimo,viwanda, madini, ujenzi, miundombinu, afya, elimu, ajira, mfumko wa bei, fedha na mabenki, mgawanyo wa bajeti katika sekta mbalimbali na kadhalika. Wabunge wamepewa Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa tarehe 14 Juni 2022 baada ya kujadili na kupitisha bajeti za sekta zote,” Aliongeza Pro Lipumba
Akizunumzia kuhusu mfumo wa bajeti, Prof. Lipumba ametaka ieleweke kuwa bajeti ya maendeleo inategemea misaada na mikopo ya ndani na nje.
Kwamba karibuni kila mwaka wa fedha mapato ya ndani hayakidhi matumizi ya kawaida ikiwa ni pamoja na kulipia madeni ya ndani na nje.
Amesema kwa mwaka wa fedha 2021/22 inatarajiwa mapato ya ndani yatazidi matumizi ya kawaida kwa shilingi bilioni 222.8 ambapo ziada ya bajeti ya kawaida itagharamia asilimia 1.7 tu ya bajeti ya maendeleo ambayo ni shilingi bilioni 13,118.4.
Hivyo ameeleza kwamba ni muhimu miradi inayoweza kutekelezwa na sekta binafsi kama vile meli za uvuvi wa kibiashara ziachiwe sekta hiyo na mashirika ya umma kama vile Shirika la Ndege la Tanzani (ATCL) yaendeshwe kibiashara.
Aidha amebainisha, Hotuba ya Bajeti haikugusa vipaumbele vya Rais vya kukamilisha na kuanza utekelezaji wa Mradi mkubwa wa LNG na pai Waziri hakujadili utekelezaji wa Ujenzi wa Bandari na eneo huria la biashara na uwekezaji la Bagamoyo.
Kuhusu ujenzi wa Demokrasia, amesema hotuba ya Bajeti haina viashiria vya utekelezaji wa upatikanaji wa katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.
“Lengo la Mkutano wa Dodoma wa kuwasilisha mapendekezo ya mkutano serikalini mapema iwezekanavyo ni maandalizi ya kibajeti yaanze kufanyika mapema na yajitokeze kwenye bajeti ya Serikali. Kuchelewa kwa Kikosi Kazi kukamilisha kazi yake kunaathiri maandalizi ya mabadiliko muhimu kama kweli kuna utashi wa kisiasa wa kuayatekeleza,” ameeleza Prof. lipumba.
Amebainisha kuwa katika Awamu ya Nne, iliamuliwa kwamba Hotuba ya Bajeti isianze bali iwe ya mwisho baada ya kujadili Bajeti za Idara na Wizara za Serikali huku Wabunge wakiwa hawapewi Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa.
“Miaka ya 1960 na 1970, wakati Kitabu hiki kinachapishwa kwa kiingereza kilikuwa na jina la Economic Survey: Background of the Budget. Uchambuzi wa Hali ya Uchumi ndiyo unaiongoza Serikali katika kuandaa bajeti inayowasilishwa Bungeni,” amefafanua Prof. Lipumba na kuongeza,
“Ili Wabunge wajadili vizuri Bajeti wanahitaji kuwa na kitabu kinachochambua maendeleo ya Uchumi ya Sekta zote, kilimo,viwanda, madini, ujenzi, miundombinu, afya, elimu, ajira, mfumko wa bei, fedha na mabenki, mgawanyo wa bajeti katika sekta mbalimbali na kadhalika. Wabunge wamepewa Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa tarehe 14 Juni 2022 baada ya kujadili na kupitisha bajeti za sekta zote,”.
Akizunumzia kuhusu mfumo wa bajeti, Prof. Lipumba ametaka ieleweke kuwa bajeti ya maendeleo inategemea misaada na mikopo ya ndani na nje.
Kwamba karibuni kila mwaka wa fedha mapato ya ndani hayakidhi matumizi ya kawaida ikiwa ni pamoja na kulipia madeni ya ndani na nje.
Amesema kwa mwaka wa fedha 2021/22 inatarajiwa mapato ya ndani yatazidi matumizi ya kawaida kwa shilingi bilioni 222.8 ambapo ziada ya bajeti ya kawaida itagharamia asilimia 1.7 tu ya bajeti ya maendeleo ambayo ni shilingi bilioni 13,118.4.
Hivyo ameeleza kwamba ni muhimu miradi inayoweza kutekelezwa na sekta binafsi kama vile meli za uvuvi wa kibiashara ziachiwe sekta hiyo na mashirika ya umma kama vile Shirika la Ndege la Tanzani(ATCL) yaendeshwe kibiashara.
Aidha amebainisha, Hotuba ya Bajeti haikugusa vipaumbele vya Rais vya kukamilisha na kuanza utekelezaji wa Mradi mkubwa wa LNG na pai Waziri hakujadili utekelezaji wa Ujenzi wa Bandari na eneo huria la biashara na uwekezaji la Bagamoyo.
Kuhusu ujenzi wa Demokrasia, amesema hotuba ya Bajeti haina viashiria vya utekelezaji wa upatikanaji wa katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.
“Lengo la Mkutano wa Dodoma wa kuwasilisha mapendekezo ya mkutano serikalini mapema iwezekanavyo ni maandalizi ya kibajeti yaanze kufanyika mapema na yajitokeze kwenye bajeti ya Serikali. Kuchelewa kwa Kikosi Kazi kukamilisha kazi yake kuna athiri maandalizi ya mabadiliko muhimu kama kweli kuna utashi wa kisiasa wa kuyatekeleza,” Alisema Prof. lipumba.
Kwa upande wa hotuba ya bajeti kuwa ndefu sana, Prof. Lipumba amebainisha kuwa hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Fedha haikuendeleza taswira ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kujenga maridhiano na umoja wa kitaifa.
Alisema hotuba hiyo ilijikita zaidi katika kupigia debe Chama cha Mapinduzi (CCM) kuliko uchambuzi wa kina wa sera za bajeti zitakazo ongeza kasi ya kukua uchumi utakao wanufaisha wananchi wote ambapo amesema ilikuwa na maelezo mengi ya vijiweni kuliko uchambuzi mahiri.
“Kitabu cha hotuba ya bajeti kina kurasa 278. Kati ya hizo kurasa 169 ni hotuba na 109 ni viambatisho. Waziri alichukua muda mrefu kueleza mambo mengi ambayo yalielezwa au yalipaswa kuelezwa kwenye hotuba za Wizara. Kauli kama hii “Tunao uwezo wa kupangua safu nzima ya utumishi wa umma na tukapanga safu mpya ya vijana hawa walioko mtaani.”
Amesema suala hili lilipaswa kujadiliwa kwenye Wizara inayohusika na Utumishi wa Umma na kuhoji ni Serikali gani inayoendeshwa kwa kuheshimu sheria na kanuni inayoweza kupangua Watumishi wote wa Umma na kuchukua walioko mtaani.
Alitoa mfano wa kauli nyingine kuwa ni “Aidha, eneo la Mtanana ambapo huwa tunasumbuka kuweka madaraja pale maji yanapokata barabara tuweke Bwawa kubwa ili bonde lote liwe la “outgrowers” wa alizeti.” Hivyo alihoji Je? Waziri anaelezea mradi wa kujenga bwawa Mtanana kwa kilimo cha alizeti cha umwagiliaji! au ni maelezo ya kijiweni?.
Prof. Lipumba ameeleza kwamba malengo mengine yameelezwa bila kufanyiwa tathmini, alitoa mfano “kuongeza thamani ya mauzo ya mazao nje ya nchi kutoka dola za Marekani bilioni 1.2 hadi zaidi ya dola za Marekani bilioni 5 ifikapo mwaka 2030 ili kuongeza uhimilivu wa deni la Taifa. Serikali inakusudia kuongeza mauzo ya Mazao ya Bustani (Horticulture) kutoka dola za Marekani milioni 750 kwa mwaka hadi dola za Marekani bilioni 2 mwaka 2030.”
Alieleza kuwa Jedwali A katika Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa 2021 ambacho Waziri wa Fedha alikizindua asubuhi ya siku ya bajeti, linaonyesha mauzo ya mazao asilia ya kilimo, na mboga na maua yamepungua toka dola za Marekani milioni 1206.5 mwaka 2016 na kufikia dola milioni 1000.7 mwaka 2021.
Hivyo ili mauzo ya nje ya sekta ya kilimo yafikie dola bilioni tano mwaka 2030 inahitajika kila mwaka ukuaji uongezeke kwa asilimia 19.6.
“Hata kama mauzo ya mazao ya kilimo ni dola milioni 1200 mwaka 2021 ukuaji wa uuzaji kwa mwaka inabidi uwe asilimia 17.2. Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa 2021 kina onyesha mauzo ya Mazao ya Mboga na Maua mwaka 2021 ni dola milioni 373 na siyo milioni 750. Hivi kweli Waziri hakuwapa Wataalam wapitie na kusahihisha makosa ya wazi,” amesema.




