Breaking News

RC SENDIGA: IRINGA IMETOA ZAIDI YA BILIONI 4 KUWEZESHA WANAWAKE

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Queen Sendiga kaifafanua jbo katika mkutano wa baraza la Wanawake la Mkoa wa Iringa ambapo pia limehudhuriwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), Gaudentia Kabaka.

Iringa:
MKUU wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Queen Sendiga amesema Serikali ya Mkoa wa Iringa imetoa zaidi ya shilingi bilioni kwenye mfuko wa akina mama wa asilimia nne na wamejipanga kuhakikisha mwaka ujao wa fedha wataongeza zaidi ya hapo.

Akizungumza katika baraza la Wanawake la Mkoa wa Iringa ambapo pia limehudhuriwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), Gaudentia Kabaka

Mhe. Sendiga amesema Serikali ya Awamu ya Sita imefanikiwa kuwatua ndoo wanawake wa Mkoa wa Iringa kwa kuleta miradi mingi ya maji kwenye kila wilaya na halmashauri zake.

Alisema Iringa bado kuna changamoto ya ukatili wa kijinsia hivyo serikali ya Mkoa wa Iringa kupitia Polisi na Mahakama imeanza kushughulikia kesi za ubakaji na ulawiti na kisha kuwafunga watuhumiwa wote ambao wamekuwa wanafanya vitendo vya kikatilii.

"Nitoe wito kwa wananchi wa Mkoa wa Iringa kuacha mara moja tabia ya kuwaficha watu ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa sababu nao watashughulikiwa na serikali kama watuhumiwa wengine" Alisema Mhe. Sendiga.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), Gaudentia Kabaka amewapongeza viongozi wa mkoa huo kwa kuendelea kushirikiana kwa ajili ya kuwahudumia wananchi ili kuharakisha maendeleo.

"Nitumie fursa hii kuwapongeza sana Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Sendiga na ndugu, Happynes Seneda (RAS) kwa ushirikiano wenu mkubwa wa kazi ambao unathibitisha manafanya kazi nzuri na yenye tija kubwa ndani ya Mkoa wa Iringa, hivyo endeleni kushirikiana nasi kama UWT Taifa tunaziona na tutawasemea vizuri kubwa endeleeni kuchapa kazi huku mkishirikiana na CCM mkoa," Alisema Mhe. Kabaka.