RC MAKALLA: AAGIZA WAKANDARASI WA TAKA, MAWAKALA NA WATUMISHI 19 JIJI KUREJESHA BILIONI 10
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa muda wa siku 60 kwa Wakandarasi wa taka, Wakala wa ukusanyaji mapato na Watumishi 19 wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam waliohusika kuchota zaidi ya Shilingi Bilioni 10 za Mapato kuhakikisha wanazirejesha fedha hizo na endapo watakaidi kutekeleza agizo Hilo watafikishwa Mahakamani.
RC Makalla maelekezo hayo wakati wa Kikako Cha baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ambapo pia ametoa muda wa siku Saba kwa Mkurugenzi wa Jiji, Mkaguzi wa ndani, msimamizi wa mfumo wa mapato na Mhasibu kutoa maelezo ya kimaandishi kueleza ni kwanini wameshindwa kudhibiti ubadhirifu wa fedha hizo.
Hatua hiyo imekuja Baada ya Ukaguzi maalumu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali CAG mwaka 2020/2021 kuonyesha kiasi Cha Shilingi Bilioni 10 zilikusanywa lakini hazionekani kwenye mfumo ambapo Wakala wamehusika na upotevu wa Bilioni 4.5 na Watumishi 19 wa Halmashauri kuhusika na upotevu wa Bilioni 5.4 na mpaka Sasa hakuna aliechukuliwa hatua licha ya CAG kuelekeza fedha hizo kurejeshwa.Aidha RC Makalla ameagiza Baada ya wahusika hao kuhojiwa, Baraza la Madiwani liliketi na kupitia upya kasoro zote zilizoonekana na kutoka na maazimio ya kuzitatua.





