Breaking News

TMDA: WANANCHI TOENI TAARIFA PINDI WANAPOPATA MAUDHI JUU YA MATUMIZI YA DAWA

Afisa mwandamizi Elimu kwa Umma na huduma kwa wateja TMDA Roberta Feruzi akielezea shughuli za TMDA kwa mkuu wa wilaya ya Tanga,Hashim Mgandilwa alipotembelea banda lao, kushoto ni Afisa Elimu kwa Umma na huduma kwa wateja Sigifrid Mtei
Afisa mwandamizi elimu kwa Umma na huduma kwa wateja TMDA Roberta Feruzi akielezea shughuli za TMDA kwa mkuu wa wilaya ya Tanga,Hashim Mgandilwa alipotembelea banda hilo.


Tanga
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)imesema kuwa inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuwa waendelee kutoa taarifa pindi wanapopata maudhi kwenye matumizi ya dawa mbalimbali.

Afisa mwandamizi Elimu kwa Umma na huduma kwa wateja TMDA Roberta Feruzi ameeleza kuwa TMDA imeanzisha mpango maalum wa kufanya ufuatiliaji katika maudhi mbalimbali katika jamii.

"TMDA ilianzisha mpango maalum wa ufuatiliaji madhara (maudhi) yanayotokana na matumizi ya dawa au vifaa tiba, hapa tunawapa elimu watu ili watoe taarifa juu ya maudhi(madhara)kwa kuwa dawa zote ni salama, lakini inawezekana ukapata reaction sio kitu kibaya hivyo kutoa taarifa ni muhimu"alisema Roberta

"Eneo la kwanza tunafuatilia madhara yanayoweza kutokana na matumizi ya dawa,watu wengi wamekuwa wakipata matatizo kwa matumizi ya dawa,lakini watu walikua hawajui watoe taarifa wapi,kwa hiyo serikali kupitia TMDA ilianzisha mpango maalum wa ufuatiliaji madhara (maudhi) yanayotokana na matumizi ya dawa au vifaa tiba,hapa tunawapa elimu watu watoe taarifa juu ya maudhi kwa kuwa dawa zote ni salama, lakini inawezekana ukapata reaction sio kitu kibaya hivyo kutoa taarifa ni muhimu" Alisema Roberta.

Roberta aliongeza kuwa katika kuhakikisha taarifa zinakuwa sahihi,Serikali imeweka mfumo wa kujaza fomu ambazo zitakua zinajazwa na mtoa huduma kama kuna madhara yaliyotokea.

Tunafanya ufuatiliaji wa madhara yanayotokana na zao la tumbaku, vuta sigara lakini vuta katika maeneo maalum, vuta sigara lakini isiwe chini ya miaka 18, usifanye promotion ya sigara kwenye mabango makubwa na kuandika maelezo ya kutokuruhusiwa chini ya miaka. 18 kwenye kibebeo cha sigara"alisema Roberta