Breaking News

MHE. KIMBISA AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUFUNGUA NCHI

Na Timothy Marko
Meya Mstaafu Adamu kimbisa amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufungua Nchi Katika kukuza Sekta ya Utalii.

Akizungumza na katika Maadhimisho ya Mahusiano ya jiji la Hurmbag na Jiji Dar es Salaam, Mheshimiwa Adamu kimbisa amesema uhusiano wa jiji la Hurmbag na Dar es Salaam katika umejikita zaidi kwa miaka mingi katika kukuza Sekta ya Utalli.

Alisema watendaji wajiji wanao wajibu wa kuhakikisha wanawekeza kukuza Sekta ya Utalli Kama alivyofanya Rais Samia Suluhu katika kukuza utalii.

"Nitoe rai kwa watendaji wote wa pande hizi mbili kuhakikisha kuwa wanakuwa mstari wa mbele katika kusaidia kutangaza fursa zilizopo na kukuza sekta ya utalii" Alisema Mhe. Kimbisa

Kwa upande wake Mayor wa jiji la Hurmbag Dr. Peter Tschentscher amesema jiji Hilo litaendelea kushirikiana na na jiji la Dar es Salaam katika kuboresha Miradi Mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.