ADC YATAKA UWAZI MKATABA WA UWEKEZAJI BANDARI ZANZIBAR
Mwenyekiti wa Chama cha Alliance Democratic Change (ADC), Taifa Hamad Rashid akizungumza wakati akifungua Mkutano wa siku moja wa Bodi ya Uongozi ya Chama Taifa jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance Democratic Change (ADC) Doyo Hassan Doyo akiwasilisha mada katika ufunguzi wa Mkutano wa siku moja wa Bodi ya Uongozi ya Chama Taifa jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa mkutano wa bodi ya uongozi wa chama cha ADC wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa.
Dar es salaam;
Chama Cha Alliance Democratic Change (ADC) kimemtaka Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hessen Mwinyi kuweka wazi mkataba wa uwekezaji wa Bandari ya Zanzibar.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Bodi ya Uongozi ya chama hicho Mwenyekiti wa ADC Taifa, Hamad Rashid ipo haja kwa dkt. Mwinyi kifata mfano wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka wazi mkataba kati ya serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na DP World katika uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
“Chama cha ADC tumeshuhudia na kuona uwazi katika mkataba kati ya serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania na DP World, tunaomba uwazi huo huo ufanyike kwenye Mkataba wa uwekezaji wa Bandari ya Zanzibar,” Alisema Rashid.
Alisema kufatia kiwepo na uwazi katika mkataba huo kati ya serikali na DP world chama kwa kauli moja tunampogeza mheshimiwa Rais Samia na pia kutoa wito kwa Rais mwinyi kufata mfano huo.
Awali akizungumzia mipango ya chama hicho kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na badae uchaguzi mkuu mhe Hamad amewataka Watanzania kujiunga na Chama hicho kwani ndio chama makini na chenye sera zinazotekelezeka kuwawezeaha wananchi na Tanzania kwa ujumla ikiondokana na umasikini.
Aidha Mwenyekiti huyo amemuomba Rais Samia kuhakikisha mapendekezo yote ya kikosi Kazi yanatekelezwa hususani tume huru ya uchaguzi ili uchaguzi ujao uwe wa huru na wazi hili kisaidia kuwezesha kupata viongozi
Akielezea kuhusu mgogoro wa mashariki ya kati unavyoendelea baina ya Israel na Palestina ameomba Jumuiya za Kimataifa hususan Umoja wa Mataifa (UN) kuingilia Kati na kukomesha mgogoro huo kwa pande mbili hasimu kukaa meza moja na kupata Suluhu ya mgogoro huo.
Hivyo kutokana na vita hiyo ametoa tahadhari kwa viongozi kuhakikisha kila Wilaya inakuwa na Hifadhi ya chakula cha kutosha.
Mapema akizungumza wakati akimkaribisha mwenyekiti, Katibu Mkuu wa Chama hicho Doyo Hassan Doyo amesema Chama kimejipanga kuhakikisha kinashika Dola katika uchaguzi mkuu ujao wa 2025.
Alisema wamedhamiria kukijenga Chama imara ambacho kitahakikisha kinaleta ushindani kwa vyama vingine.
Aidha Doyo amelaani kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda kusema kwamba hakuna Vyama vya upinzani nchini.
“Tunalaani kauli ya Makonda kwamba hakuna Vyama vya siasa vya upinzani. Hii nidharau kwa Masajili wa Vyama vya Siasa,” Aloema Doyo.






