BAADA YA MIEZI ZAIDI YA MITANO WARDA APATIKANA, AKABIDHIWA KWA MAMA YAKE MZAZI, MAPITO AFRICA FOUNDATION YAMUAHIDI
Mtoto Warda Mohamed baada ya kukutanishwa na mama yake Mzazi bi. Sakina Mtalika kufatia kutoweka kwake zaidi ya miezi mitano jijini Dar es salaaam
Mkurugenzi wa Mapito Afrika Foundation Zaliam Tabuyanjaa akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa Habari mara baada ya kupatikana mtoto warda jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Chamazi Federation, bwana John Ernest akielezea namna alivyopata taarifa za kupotea kwa mtoto warda jijini Dar es salaam.
Mtoto warda akizungumza kilichotokea mpaka yeye kutoweka takribani miezi mitano mara naada ya kipatikana na kukutanishwa na wazazi wake jijini Dar es salaam.
Dar es salaam
Takribani zaidi ya miezi mitano tangu kutoweka kwa mwanafunzi wa Kidato cha Pili wa Shule ya Sekondari Nyumbu iliyopo Kibaha Mkoani Pwani, Warda Mohamed (16) amepatikana siku ya tarehe 28 oktoba Chamazi Federation jijini dar es salaam na leo kukabidhiwa kwa famlia yake.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Taasisi ya Mapito Africa Foundation Zaliam Tabuyanjaa ambaye ni mratibu wa kampeni ya "YUKO WAPI WARDA" amesema usiku wa Oktoba 28, 2023 ndio alipokea taarifa kutoka kwa msamalia melwema kuhusu kupatikana kwa Warda akiwa anaishi na msamalia mwema Chamazi Federation.
“Tangu tuanze zoezi la kumtafuta mtoto warda kumtafuta hadi Tarehe 28 nilikuwa nimeshaanza kukata tamaa, Tunashukuru Warda amepatikana, siku ya Septemba 29 tulipopata taarifa kutoka kwa msamalia mwema kuwa amepatikana,” Alisema Bi Zaliam
Alisema Warda alipotea tangu Aprili Mwaka huu akiwa anaishi Kibaha na Mwalimu wake Sema, leo kwa mara ya kwanza tangu apatikane tumemkutanisha na mama yake pamoja na familia yake.
Zaliam aliongeza kuwa kukabidhiwa kwa warda sio mwisho bali watahakikisha kuwa wanampambania Warda kimasomo kwa kuhakikisha anakwenda Shule na kutimiza ndoto zake.
Nae mtoto Warda akizungumzia tukui hilo amesema sababu ya kuondoka bila taarifa Nyumba kwa Mwalimu aliyekuwa anaishi naye ni baada ya kurudi nyumbani akitoka Shule na kupokea kipigo kutoka kwa Mwalimu huyo pamoja na dada wa nyumbani hapo.
"Napenda kuomba radhi kwa Wazazi pamoja na ndugu zake kwa hatua hiyo aliyochukua bila kuwashirikisha jambo lilopelekea kusababisha taaruki katika familia kipindi chote cha kutokujulika a alipo" Alisema Warda.
Kwa upande wake mama Mzazi wa Warda Bi Sakina Mtalika anenza kwa kimshukuru Mungu, Kampuni ya Global Publishers kupitia kipindi cha mapito kinacho ongozwa na Zaliam pamoja na Jeshi la Polisi kwa namna ambavyo wameshiriki kuakikisha kuwa Warda anapagikana.
Alisema katika kipindi chote cha kumtafuta mtoto warda kama binadam na kulimgana na mazingira yalivyo walijukuta wanashundwa kuelewana na baadhi ya taasisi hivyo amemeomba radhi pale alipotoa kauli ambazo hazikuwa sahihi kwamba haikuwa makusudi yake bali ni kwa sababu yakutokuwa sawa kutokana na kupotelewa na mwanaye.
“Nashukuru RPC kwa kuonesha ushirikiano, pamoja na chamgamto mbalimbali ambazo zilitokeza katika kipindi chote cha kumtafuta mtoto warda leo nafurahi kwa kupatikana Mwanangu,” Alisema Sakina.
Naye Msamalia aliyekuwa anaishi na Warda, bi. Schola Leonard mkazi wa Chamazi Magengeni amesema Warda aliletwa nyumbani na Mwanaye aliyekuwa akitoka kazini baada ya kumuona katika Mazingira hatarishi kwa maisha yake.
Mara baada ya kufika tu alichukua hatua ya kumpeleka kwa Mjumbe na kisha kwenda Polisi kuripoti ndipo ilipoamuliwa aishi naye hadi wazazi au ndugu zake watakapopatikana.
Kwa upande wake Mjumbe wa Chamazi Federation, bwana John Ernest amesema alipewa taarifa za kuonekana kwa Warda ambaye alikuwa amepotea Aprili Mwaka ambapo anakumbuka siku hiyo ilikuwa ni majira ya Saa 6 usiku.







