Breaking News

MARUFUKU MTU ASIYE NA TIKETI KUFIKA UWANJA WA BENJAMINI MKAPA MECHI YA SIMBA NA AL AHLY

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku mtu asiye  na tiketi kufika Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya uzinduzi mashindano “African football league” uzinduzi utakao enda sambamba na mchezo wa kwanza hatua ya robo fainali kati ya timu ya Simba ya Tanzania na Al Ahly kutoka nchini Misri majira ya saa 12:00 jioni.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Muliro Jumanne Muliro ametoa kauli hiyo wakati akizungumzia maandalizi ya ufunguzi wa mashindano hayo na kuelekea mechi hiyo Jijini Dar es Salaam.

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limejipanga kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi kuhakikisha siku hiyo ya ufunguzi wa mashindano “African football league” unafanyika kwa amani kuanzia kabla ya mechi na mara baada ya mechi" Alisema SACP Muliro.

Alisema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi wanatambua kuwa mchezo huo ambao kutachezwa katika uwanja wa Mkapa ni mkubwa katika kuhakikisha kuwa unafanyika kwa ufanisi baadhi ya barabara zitafungwa kwa lengo la kupunguza msongamano kuelekea na kutoka uwanjani hivyo mashabiki wa soka wafike mapema wakila na tiketi zao hili kuepusba usumbufu unaoweza kuepukika.

"Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi wamechukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati wa mchezo na baada ya mchezo huo ukaguzi wa hali ya juu katika mageti ya kuingia na mtu yeyote aruhusiwi kwenda uwanjani na silaha ya aina yoyote, isipokuwa baadhi ya vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo" Alisema SACP Muliro.

Aiddha SACP Muliro ametoa rai kwa mashabiki wenye tabia ya kuwasha fataki au baruti uwanjani, hayo ni baadhi ya makosa ya mambo ya kiusalama kwenye viwanja vya soka hivyo Jeshi la Polisi halitavumilia tabia hizo na zingine ambazo zimepigwa marufuku  na  vyama vya soka FIFA, CAF na TFF tabia ambazo zinaweza kupelekea Tanzania kukosa sifa ya kuandaa mashindano kama haya wakati mwingine.