SIMBA SC, AZAM FC NA SINGIDA FOUNTAIN GATE KUSHIRIKI KAMPENI YA KUTOKOMEZA UKATILI KWA WANAWAKE NA WATOTO
Naibu Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni Hamisi Mwinjuma akiifafanua jambo katika hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Thamani Women Tanzania Bi.Nafue Nyange akielezea namna ambavyo kampeni hiyo ya Kitaifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto hafla iliyoganyika katika hotel ya Hyatt' Kilimanjaro hotel Jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam:
Taasisi ya Thamani Women Tanzania imezindua rasmi kampeni ya kitaifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto inayojulikana kama ‘Piga Mpira Sio Mwanamke’.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni, Hamisi Mwinjuma ameesema kupitia kampeni hiyo ambayo imeshirikiana na klabu za Simba SC, Azam FC na Singida Fountain Gate FC inatoa faraja hususani kwa wazazi na walezi nchini.
"Niwapongeze waandaaji wa kampeni hii kwa kuamua kushirikisha hivi vilabu kwani huwa tunaviona uwanjani vikipambana kwa ajili ya ushindi wa ligi kadhaa. Kama si Ngao ya Jamii basi, NBC Premier League au league nyingine,” Alisema Mhe. Mwinjuma.
Alisema Michezo imekuwa na uwezo na nafasi kubwa sana ya kuwaunganisha watu au jamii kutokana na kuwa na nguvu kubwa katika miktadha yote. Bila kujali kiwango cha taaluma ya juu kabisa mpaka chini, watu wenye vipato tofauti, matabaka na dini tofauti. Michezo ina njia ya kuunda hali ya jamii pia.
“Kwa mfano, ukifuatilia Soka la hapa Tanzania na hata ligi za nje, unaweza kuona jinsi mashabiki walivyo na uwezo wa kushikamana mara moja na shabiki ambaye wamekutana naye hivi karibuni wa timu moja,” Alisema Mhe. Mwinjuma
Alisema kupitia michezo hususani mpira wa miguu umekuwa ukiwaleta pamoja watu na jamii kupitia uundaji wa mashujaa na, kadiri shujaa anavyo-jihusisha zaidi na jamii, ndivyo muunganisho unavyokuwa thabiti.
Kampeni hii kutumia mchezo wa mpira jambo la kuungwa mkono na kupongezwa pia kutokana na mchezo kuwa na zana muhimu ya kuvunja vizuizi vya kijamii na kitamaduni nje ya uwanja wachezaji kutoka nyanja mbalimbali wana jukumu la kufanya kazi pamoja kufikia lengo moja ushindi dhidi ya timu pinzani.
“Siku ya Leo tunashuhudia kupitia vilabu hivi vitatu vikubwa nchini vikiungana dhidi ya mpinzani mmoja ukatili ni jambo jema na pia ni jambo la faraja” Alsema mhe. Mwinjuma.
Alisema takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 40 ya wanawake wenye umri wa miaka 15-49 wameshakutana na adha ya ukatili wa kimwili, Asilimia 17 tayali wmefanyiwa ukatili wa kijinsia huku
asilimia 44 ya wanawake wenye miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili au kijinsia na wenza wa karibu.
Mhe Mwijuma aliongeza kuwa kwa kipindi kirefu swala la kupinga ukatili limekuwa likiongelewa na wanawake, hivyo ni wakati muafaka wa vijana wa kiume, kina baba wa makamu tofauti kulijadili janga hili la kitaifa ili kurithisha watoto Taifa lenye utulivu, amani, upendo na maendeleo kwani Wanawake wana mchango mkubwa sana katika maendeleo ya Taifa na maendeleo ya wanaume kwa ujumla.
Aidha Mhe. Mwijuma ameitaka jamii kujitokeza na kuunga mkono bidii na hatua mbalimbali zinazo chukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita pamoja na Taasisi ya Thamani Women Tanzania katika kuwa tumatokomeza vitendo hivi katika jamii.
Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Thamani Women Tanzania, Bi Nafue Nyange amesema lengo la kampeni hiyo kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa jinsia zote mbili pamoja na mageuzi ya sheria zinazo athiri wanawake na watoto.
“Sambamba na uzinduzi wa taasisi tunazindua rasmi kampeni ya kitaifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake hali kadhalika watoto, Mama akinyanyasika mtoto anadhoofika kama si afya ya mwili basi ya akili,” amesema Nyange.
Amesema asilimia 58 ya wanawake na asilimia 40 ya wanaume wanaamini kwamba mume ana haki ya kumpiga mke wake palipo hali fulani ambapo asilimia 54 pekee ya wanawake nchini Tanzania waliofanyiwa ukatili wa kimwili au kingono wanatafuta msaada kwenye vyombo vya usalama,au kwa viongozi wa familia.
Naye aliyekuwa Mbunge Mstaafu wa Tabora Mjini mheshimiwa Ismail Rage ameipongeza Taasisi ya Thamani Women Tanzania kwa hatua yao ya kuanzisha kampeni hiyo nchini.
Alisema pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali katika kuhakikisha kuwa wanatokomoza ya ukatili wa kijinsia katika jamii kupitia kampeni hii inatia amasha kwa kuzingatia ushirikj wa vialabu vikubwa vya mpira hapa nchini itasaidia kuwafikia jamii kwa wepesi.
"Niwapongeze kwa hatua hii ya kuzindua kampini ga kutokomeza ukatili wa kijinsia pia wanaume tutambue kuwa kitendo cha kumpiga Mwanamke mabango ya kampeni yawekwa katika viwanja vyote vya mpira ili kusaidia elkmu hiyo inamfikia kila mtu" Alisema Bw. Rage.
Mapema wawakilishi kutoka timu za Simba SC, Azam FC na SINGIDA FOUNTAIN GATE wakizungumza katika uzinduzi huo wamesema klabu hiyo pamoja na Wachezaji wake inatambua adhali za ukatili wa kijinsia katika jamii hivyo kuwaakikishia waandaaji wa kampeni hiyo kuwa watahakikisha wanashirika vyema hili kuiwezesha kuwafikia kwa wananchi.



.jpg)



